Tafuta

Usomaji wa Kuran wakati wa kiipindi cha  Ramadhani Usomaji wa Kuran wakati wa kiipindi cha Ramadhani  

Ujumbe wa Kard.Sako kwa matashi mema ya Mfungo wa Ramadhani

Katika mfungo wa Ramadhani ulionza tarehe 13 Aprili kwa Waislamu,matashi mema ya Patriaki wa Kikaldayo katika ujumbe wake ni kuwa Radhamani iwe kipindi cha kukaribia sana Mungu na watu kwa njia ya mfungo,sala,matendo ya upendo na huruma,msamaha na upatanisho,pamoja na kujikita kwa kina kutengeneza uhusiano wa kidugu,urafiki na heshima ambayo Papa aliwakumbusha katika ziata ya Kitume Iraq.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe wa Patriaki wa Kikaladayo wa Baghdad, Kardinali Louis Raphael Sako, kwa waislamu kwa ajili ya mwanzo mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa kufunga na kusali ambao umeanza tarehe 13 Aprili 2021, na utahitimishuwa Jumatano tarehe 12 Mei 2021, anawatakia matashi mema ya dhati na Baraka kwa ndugu hao huku akiomba Mungu mwenyezi abariki mfungo wao na kuwapa afya na usalama na kuwaepusha hatari za janga la Covid-19”.

Matashi mema ya Patriaki ni kuwa Radhamani iwe kipindi cha kukaribia sana Mungu na watu kwa njia ya mfungo, sala, matendo ya upendo na huruma, msamaha na upatanisho, pamoja na kujikita kwa kina kutengeneza uhusiano wa kidugu, urafiki na heshima ambayo Papa Francisko aliwakumbusha wakati wa ziara yake ya Kitume iliyofanyika hivi karibuni nchini  mwao Iraq.

Patriaki Sako amesema “Kipindi hiki kiweze kuwa hata cha kuhamasisha misingi ya amani, msimamo na kuishi pamoja ili kuweza kufungua ukurasa mpya  katika maisha ya wana Iraq. Ni kwa kuwafanya waweze kunufaika kwa furaha baada ya mabaya yote ambayo yametokea katika nchi yao. Kardinali Sako aidha anatoa ombi lake hasa la  kupitisha na kuingiza katika vitabu vya shule, kwenye fursa hii, maneno ambayo wamezoea kuseam kuwa “Watu wa Kitabu' kwa kufafanua Wakristo liwe la dhati badala ya ufafanuzi mwingine usio sahihi na usiokubalika”.

13 April 2021, 13:52