Deca - Msikiti Mkubwa Deca - Msikiti Mkubwa  

Ufaransa:Maaskofu wanawatakia matashi mema ya mfungo wa Ramadhani

Rais wa Baraza la Uhusiano wa kidini na mikondo mipya ya kidini ndani ya Baraza la Maaskofu Ufaransa katika fursa ya Mfungo wa Ramadhani ulionza tarehe 13 Aprili amendika kuwa anajua kutokana na uzoefu kwamba urafiki,heshima ndiyo injini bora kwa ajili ya mazungumzo na amani na ni urafiki ambao unatuchochea kupata ishara rahisi za mshikamano katika kuhudumia maskini zaidi katika jamii mfano:wagonjwa,wapweke,wahamiaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

“Kwa pamoja tunaweza kujizoeza kumtumikia Mungu vizuri kwa kuwahudumia ndugu kaka na dada zetu”. Kwa mwaliko huu wa kufanya kazi pamoja hasa kwa walio hatarini zaidi katika jamii, ndivyo Askofu Mkuu Jean-Marc Aveline, rais wa Baraza la uhusiano wa kidini na mikondo mpya ya kidini ndani ya Baraza la  Maaskofu wa Ufaransa(Cef), anaelezea matashi mema kwa Waislamu wa Ufaransa katika tukio la mfungo wa Ramadhani, ilioanza tarehe 13 Aprili 2021.

"Ninajua kutokana na uzoefu kwamba urafiki, heshima na unadai, ndiyo injini bora kwa ajili ya mazungumzo na amani na ni urafiki ambao unatuchochea kupata ishara rahisi za mshikamano katika kuhudumia maskini zaidi katika jamii zetu: wagonjwa, wapweke, wahamiaji”, Anaandika askofu mkuu wa Marseille. Akinukuu “Sala ya Wana wa Ibrahimu” iliyoombwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 6 Machi iliyopita wakati wa mkutano wa kidini katika Uwanda wa Uru, nchini Iraq, katika Ziara yake ya Kitume, Askofu Mkuu Aveline ameonesha kuwa udugu wa matumaini ndiyo ufunguo.

Kwa maana hiyo katika ujumbe wake anaandika kuwa:“Tumaini, ni siri ya udugu, kwa sababu inatupatia sura hiyo ya fadhila, inayoweza kupokea matendo mema ya uwepo wa Mungu kwa kila ndugu wa kibinadamu. Kwa sababu hiyo na nyinyi, tunaamini kwamba kila mtu lazima aheshimiwe, hata katika utamaduni na hali yake ya kiroho”, anaandika. Na kwa roho hiyo, kiongozi huyo kwa niaba ya Kanisa la Ufaransa ametoa matashi mema ya Ramadhani na kwamba iwe yenye amani na matunda na Id al-Fitr ya furaha.

15 April 2021, 14:03