2021.03.31 Baada ya moto uliotokea karibu na jiji la Free Town watu wengi wamebaki bila nyumba 2021.03.31 Baada ya moto uliotokea karibu na jiji la Free Town watu wengi wamebaki bila nyumba 

Sirra Leone:Caritas kusaidia waathiriwa wa moto huko Free Town

Ni watu 7000 waliorundikana na majeruhi 400 kufuatia na mlipuko wa moto uliotokea tarehe 25 Machi 2021 huko Freetown,nchini Sierra Leone.Caritas kitaifa inaendelea kutoa msaada wake hadi siku 21 kwa watu ambao wamebaki bila mahali pakujihifadhi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Moto mkubwa ulitokea huko ufukweni mwa Susan, katika mabanda ya kuishi yaliyopo pembeni mwa mji mkuu uliojengwa kwa mabati na zana  duni kabisa za kubabaisha tarehe 25 Machi 2021, na kusababisha mlundikano wa watu 7000 na majeruhi 400. Kwa taarifa ni kwamba ni karibu watu elfu 11 ambao kwa miaka mingi, wameweza ujipatia makazi huko ya  kubabaisha, huku wakijenga jumuiya kubwa hasa inayojikita katika shughuli za biashara isiyo rasmi na uvuvi. Shukrani kwa eneo hilo, kwa wastani  katika eneo hilo la Susan, ndio mahali pa kutua kwa mamia ya mitumbwi ambayo kila siku hupakua bidhaa kutoka nchi ya bara, pamoja na makaa au mboga, zinazopelekwa katika masoko ya ndani ya nchi.

Kwa sasa, ili kusaidia watu waliorundikana Caritas ya jimbo imechukua uwanja mkubwa na  imezindua mpango wa dharura uliopangwa kwa zaidi ya siku 21. Wakati huo huo, hali mbaya ya hewa ilikumba jiji hilo, huku ikileta mvua kubwa ambayo, kwa upande mmoja ilichangia kuzima moto, lakini upande mwingine, ilizidisha kuwa na hali ya watu ambao walibaki bila makazi ya aina yoyote ya kujisitiri.

Hali ni ngumu sana kwa mujibu wa Ishmeal Charles, msimamizi wa programu ya Caritas ya Freetown na kwamba hadi sasa, wanatoa wastani wa chakula kwa watu elfu 3 kila  siku katika  idadi ya wahitaji na wataendelea kufanya hivyo kwa siku 21. Ili kutekeleza misaada hiyo, vituo 7 vya kuweza kutoa msaada huo na uratibu vimewekwa. Wapo hata watu wa kujitolea wa shirika la misaada ambao huwapatia wakimbizi chakula, vyombo, maji ya kunywa, blanketi na mavazi msingi ya lazima.

Caritas kitaifa ilianzishwa mnamo 1981 na Baraza la  Maaskofu wa Sierra Leone, ambayo inazingatia  kujitolea kwake, hasa katika miaka ya 1990, katika kujibu mahitaji ya wahanga wa idadi ya watu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoharibu nchi hiyo tangu 1991 hadi 2002, kwa sababu ya vurugu na  mzozo kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Chama cha umoja wa Mapinduzi.

Katika hali halisi ya kiungo hiki cha hisani kimejikita kusaidia watoto wanajeshi huku ikijaribu kuwakomboa kutoka katika uajiri wa kulazimishwa. Leo, hii Caritas ya Sierra Leone haihusiki katika mipango ya kujenga amani tu , lakini pia hata katika miradi ya misaada kwa ajili ya idadi ya watu; kwa mfano, kazi maalum inafanywa katika uwanja wa kuzuia VVU / UKIMWI, na pia katika sekta hiyo. usalama wa chakula, kuhamasisha vijana, ulinzi wa mazingira na kutokomeza umaskini na usawa wa kijinsia.

01 April 2021, 14:12