Papa Francisko akisalimiana na Kardinali Sako wakati wa ziara yake ya kitume nchini Iraq Papa Francisko akisalimiana na Kardinali Sako wakati wa ziara yake ya kitume nchini Iraq 

Pasaka nchini Iraq:Papa ameacha ishara ya mwanzo wa ufufuko

Shukrani kwa ziara ya Papa Francisko nchini Iraq bado inasikika kwa nguvu na uhai wote.Maadhimisho ya Pasaka,yote yamezungukwa na ujumbe wa matumaini ambayo Papa aliwaachia.Ni kwa mujibu wa Patriaki wa Kikaldayo huko Baghdad Kardinali Sako akielezea juu ya barua ya shukrani kwa Papa aliyomtumia kutokana na kupokea msaada kwa ajili ya watu wa Iraq wenye shida.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Licha ya vizuizi vya kiafya, Kanisa mahalia limejitoa kusaidia familia zilizo katika shida na matumaini kwamba hewa mpya itaenea katika ardhi hiyo. majeraha hayapotei kwa viini macho; watu wenye mapenzi mema wanahitajika kurudisha hatua za Papa Fransisko. Patriaki wa Kikaldayo wa Baghdad, Kardinali Louis Raphael Sako, amerudi kuelezea katika barua aliyomtumia Baba Mtakatifu Francisko shukrani zake kwa safari ya kitume ya hivi karibuni nchini Iraq, pia kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki.

Kardinali ametangaza kwamba Papa alipenda kusaidia watu wa Iraq kwa msaada wa dhati na kwamba Upatriaki na Kanisa la eneo hilo, kwa kufuatia matakwa ya Baba Mtakatifu, tayari wamefanya kazi ya kutenga misaada ya kifedha ili kusaidia mipango ya familia zilizoathiriwa hasa  migogoro, ya shida ya uchumi na janga, familia za Kikristo na Kiislamu na  jamii nyingine zote za imani zilizopo Iraq. Patriaki amesisitiza kwamba ziara ya Papa iligusa mioyo ya raia wote, ikipanda ufahamu wa umuhimu wa kukubaliana, kuelewana na kuheshimu utofauti ili kuhakikisha utu, hadhi, uhuru na usawa wa haki na wajibu vinatendekea. “Tunatumahi kuwa njia hii ya mwenendo pia itahimiza nia wenye nguvu ulimwenguni, amesema Kardinali Sako.

03 April 2021, 16:27