Makumi kadhaa ya maaskofu wakianglikani ulimwenguni kote  wamesaini ombi siku za hivi karibuni wakitaka kusitishwa kwa haraka uchimbaji wa mafuta kwenye bonde la Kavango, nchini Namibia,kazi inayofanywa na kampuni ya Canada Makumi kadhaa ya maaskofu wakianglikani ulimwenguni kote wamesaini ombi siku za hivi karibuni wakitaka kusitishwa kwa haraka uchimbaji wa mafuta kwenye bonde la Kavango, nchini Namibia,kazi inayofanywa na kampuni ya Canada  

Namibia:Ombi la maaskofu wa kianglikani kuzuia kuchimba mafuta ili kulinda hifadhi ya asili

Maaskofu 34 nne na maaskofu wakuu watatu wametoa ombi kwa serikali ya Namibia kupitia ubalozi mdogo wa Namibia huko Cape Town na makao makuu ya kampuni ya mafuta huko Vancouver ili kuzuia uchimbaji wa mafuta katika bonde la Nambia ili kulinda hifadhi ya asili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Makumi kadhaa ya maaskofu wakianglikani ulimwenguni kote wamesaini ombi siku za hivi karibuni wakitaka kusitishwa kwa haraka uchimbaji wa mafuta kwenye bonde la Kavango, nchini Namibia, katika  kazi inayofanywa na kampuni moja ya Canada katika sekta hiyo. Hawa ni Maaskofu thelathini na nne na maaskofu wakuu watatu walitoa ombi hilo kwa serikali ya Namibia, ubalozi mdogo wa Namibia huko Cape Town na makao makuu ya kampuni ya mafuta huko Vancouver. Mpango huo umeanzia kwa Askofu Luke Pato ambaye aliwatarifu wajumbe wa Jumuiya ya kianglikani kwamba kuchimba visima vya uchunguzi kumeanza katika eneo la nchi hiyo ya kiafrika.

Kampuni ya Canada imepata haki za kuchimba mafuta katika zaidi ya kilometa za mraba 35,000 za bonde la Kavango, ambalo linasambaza maji katika bonde la Okavango, eneo ambalo ni makazi ya hifadhi ya asili na idadi ya watu asilia karibu watu 100,000.  Kwa upande wa maombi yanasomeka kuwa: “Utafiti huu unakiuka haki zilizowekwa katika tamko la Umoja wa Mataifa juu ya watu wa kiasili. Maji ni bidhaa adimu na ya thamani nchini Namibia ambayo ni nchi kavu zaidi kusini mwa jagwa la Sahara”. Kwa mujibu wa waombaji hao, ambao wanaripoti kile kilichotangazwa kwenye tovuti ya kampuni ya Canada, kuwa  “mafuta ambayo yanaweza kutolewa  kwenye bonde la Namibia yanaweza kutoa mapipa ya mabilioni, katika uwanja huo mkubwa zaidi ya mafuta katika muongo mmoja”.

Ombi la maaskofu wa kianglikani pia linataja mchakato duni wa ushiriki wa umma katika operesheni ya madini. Wasiwasi uliooneshwa na wanaharakati wa eneo hilo, ni kwa sababu waombaji pia wanalaani kwamba Gazeti la Namibia ambalo lilifunua habari hiyo, lilitishiwa kuchukuliwa hatua za kisheria. “Uchimbaji kwenye bonde la Kavango utavunja muundo wake wa kijiolojia na kuharibu mfumo wa maji unaosaidia mfumo huu wa kipekee, kuhifadhi wanyamapori”, wanaandika viongozi hao.

Kwa suala hili  pia amezungumzia Katibu mkuu wa mpito wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, Mchungaji Ioan Sauca, ambaye ameonesha mshikamano na ukaribu na watu wa Namibia na jumuiya ya Kianglikani walioshiriki katika maandamano dhidi ya uchimbaji mbaya wa mafuta kwenye bonde la Kavango. “Hatuwezi kutoa haki za jamii za wenyeji na kuharibu zawadi ya uumbaji wa Mungu kwa ajili ya mafuta”, amesema Mchungaji Sauca. “Ikiwa tunataka kufikia lengo la kimataifa la kupunguza uzalishaji wa hewa inayodhuru  watu ifikapo mwaka 2030 na kufikia kutokuwamo kwa kaboni ifikapo mwaka 2050, lazima tumalize utegemezi wetu katika  mafuta na tuchukue njia ya mpito kuelekea mifumo wa nishati mbadala kuanzia sasa”, amethibitisha mwakilishi wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni.

01 April 2021, 15:05