Tafuta

Kardinali Angelo Bagnasco Rais wa  CCEE Kardinali Angelo Bagnasco Rais wa CCEE 

Miaka 20 ya Mkataba wa Kiekumene kwa ajili ya ulimwengu wa haki na amani

Kardinali Bagnasco,rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya(Ccee)na Mchungaji Krieger,rais wa Mabaraza ya Makanisa Ulaya(Cec),wanatambua kuwa katika miaka ya hivi karibuni katika bara la Ulaya kumekuwa na kipindi cha amani,pamoja na kuboreshwa kwa uhusiano wa kiekumene.Makubaliano kadhaa ya kitaalimungu yamefikiwa na kizazi kipya cha wataalimungu kimeundwa kiekumene na mipango kadhaa ya dini imefanikiwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Jumuiya ya Ulaya iliyovukwa na mgawanyiko wa zamani na mpya, iliokabiliwa na mzozo wa janga, iliyojeruhiwa na ukosefu wa usawa kijamii na kiuchumi, Makanisa yanathibitisha kujitoa kwao kuwa vyombo vya umoja na kufanya kazi pamoja kwa kuhahamasisha haki na amani. Walifanya hivyo katika Azimio la pamoja lililotiwa saini na marais wa Baraza la Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu  Ulaya  (Ccee) na la Mabaraza  ya Makanisa ya Ulaya (Cec) wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya  Mkataba wa Kiekumene (Charta Oecumenica).

Hati ilisainiwa Aprili 22, 2001

Hati  hiyo ilisainiwa huko Strasbourg mnamo tarehe 22 Aprili 2001 na bado leo hii inawakilisha kuwa hati msingi ambayo inataka kuhifadhi na kukuza udugu kati ya makanisa ya Ulaya. Kwa kufanya hesabu ya miaka 20 iliyopita, Kardinali Angelo Bagnasco, rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu  Ulaya  (Ccee), na Mchungaji Christian Krieger, rais wa Mabaraza ya Makanisa Ulaya (Cec), wanatambua kuwa katika miaka ya hivi karibuni katika bara la Ulaya kumekuwa na kipindi cha amani, pamoja na kuboreshwa kwa uhusiano wa kiekumene. “Makubaliano kadhaa ya kitaalimungu yamefikiwa na kizazi kipya cha wataalimungu ambacho kimeundwa kiekumene; na mipango mbali mbali ya dini imefanikiwa.

Mafanikio ya hati ya pamoja

Makanisa yameimarisha kazi yao kuelekea ulimwengu wa haki na amani, sio hiyo tu pia sababu ya kuongezeka kwa harakati za watu kutoka mabara mengine na wameongeza juhudi zao kwa utunzaji wa kazi ya uumbaji. Yote haya pia yametokana na Hati ya Makubaliano ya Kiekumene ambayo ilichangia na kutoa nguvu mpya kwa ukuaji huu wote na mabadiliko. Walakini, licha ya maendeleo yaliyofanywa, makanisa na jamii za Ulaya bado zinaendelea kupingwa na kila aina ya mgawanyiko. “Mgawanyiko wa zamani na mpya katika Kanisa kwa mujibu wa Azimio zinahitaji uponywaji, usawa wa kijamii na kiuchumi lazima kuwa na mabadiliko ya mitazamo yetu na miundo yetu”.

Vitisho vua kidemokrasia na uhitaji wa uongofu

Vitisho vya mara kwa mara vya kidemokrasia na mazingira ya asili vinahitaji umakini mpya kwa ujumla wa maisha. Kuibuka tena kwa mizozo ya silaha na mashambulio ya kigaidi katika sehemu nyingine za bara katika miaka ya hivi karibuni vinahitaji uongofu wa  kweli, msamaha na haki”.  Katika Azimio hilo, marais pia wanataja changamoto ya janga la Covid-19 na wanathibitisha tena kujitolea kwao ili kumshuhudia Kristo kama Mwokozi wetu na ahadi yake ya maisha yaliyobadilishwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Afla itafanyika tarehe 22 Aprili kwa njia ya mtandao

Kwa muktadha huo viongozi hawa wanapenda kuwa vyombo vya umoja huo na kujitoa tena kuimarisha muungano wa kikanisa kwa njia ya sala ya pamoja na matendo ya pamoja wakati huo huo wakitoa huduma yao kwa ulimwengu ili kuhamasisha haki na amani. Katika muktadha wa sherehe za maadhimisho haya, CCEE na Cec wameandaa tarehe 22 Aprili 2021, kuanzia saa 1.00 hadi 2:30 usiku, kufanya tukio moja la kiekumene kwa njia ya mtandao itakayoongozwa na kauli mbiu “Furahini katika tumaini, subira katika mateso, kwa kusali na kuomba. Kwa kutaka kufuatilia afla hiyo unaweza kubonyeza hapa:link: https://zoom.us/webinar/register/WN__lClRISEQW2ofhF2ufA0aA Au kufuatilia kupitia YouTube: https://www.youtube.com/channel/UCmNjQop8IRofn3WO4mIDLzg.

14 April 2021, 13:04