Tafuta

WAAMINI MBELE YA KANISA HUKO IVORYCOAST WAAMINI MBELE YA KANISA HUKO IVORYCOAST 

Ivory Coast,Siku ya Kitaifa ya Wafungwa:Kanisa limeonesha ukaribu!

Kanisa nchini Ivory Coast linahimiza mamlaka ya umma kuzingatia hasa vituo vya kuwekwa watu kizuizini kabla ya kesi ambavyo sehemu kubwa inakabiliwa na hali ya wasiwasi wa msongamano wa watu,wapewa msamaha kutoka kwa rais wa nchi.Ni katika muktadha wa Siku ya kitaifa ya wafungwa nchini humo hivi karibuni ambapo Kanisa limeelezea ukaribu wake wa dhati.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kila mwaka nchini Ivory Coast, kwenye sikukuu ya Huruma ya Mungu, Kanisa huadhimisha Siku ya Kitaifa kwa ajili ya Wafungwa, iliyoanzishwa na mpango wa Tume ya Maaskofu ya Haki, Amani, Mazingira Kitaifa na  uchungaji katika magereza. Maadhimisho rasmi ya toleo la 2021 iliongozwa na kaulimbiu “Utunzaji wa Kanisa kwa ajili ya wafungwa ni njia ya uongofu na amani, ambayo ilifanyika Jumapili iliyopita tarehe 11 Aprili 2021, kwa kufanya maadhimisho ya Misa takatifu ikiongozwa na Askofu Mkuu Joseph Yapo Aké, wa Gagnoa, katika Parokia ya Watakatifu Petro  na Paulo  wa Divo (Katikati-Magharibi) ya Jimbo kuu la Gagnoa.  Katika hotuba yake, akizungumza kwa niaba ya Askofu Bruno Essoh Yedo, Askofu wa Bondoukou (Kaskazini-Mashariki) na Rais wa Tume ya Haki na Amani, Padre Charles Olidjo Siwa, Katibu Mkuu wa Tume na mchungaji wa kitaifa kwa ajili ya utunzaji wa wachungaji wa magereza mbele ya viongozi wa kisiasa na kiutawala wa nchi hiyo, alielezea kutambuliwa kwa Kanisa juhudi zilizofanywa kwa wafungwa, lakini pia hata kuelezea wasiwasi wake juu ya msongamano katika maeneo ya vizuizini.

Katibu huyo alisema kuwa “Kanisa linahimiza mamlaka ya umma kuzingatia hasa vituo vya kuwekwa watu kizuizini kabla ya kesi ambavyo sehemu kubwa inakabiliwa na hali ya wasiwasi wa msongamano wa watu”.  “Kituo cha kutunza watu kabla ya kesi na marekebisho cha Abidjan, ambacho kina uwezo wa wafungwa 2000, kwa sasa kina wafungwa zaidi ya 7000 na hali hii inadhoofisha sana hadhi ya mwanadamu ambaye lazima atunzwe kila wakati na kila tukio”. Akiendelea kusoma  ujumbe huo wa  Siku ya Kitaifa ya Wafungwa amesema  Kanisa linaomba mamlaka ya umma kwamba lifanyike tendo la kuwaachia huru yani msamaha mbele ya watu ambao wanajikuta wako kizuizini na ambao wanaweza kufaidika na neema hiyo kutoka kwa rais.

Vile vile Kanisa linatambua katika ujumbe wake kwamba karibu vituo vyao  vyote vyenye wafungwa, kuanza kesi na mahabusu wanakosa muundo wa mafunzo hasa kwa mahali pa kijifunzia shughuli za biashara ambayo ingeweza kuwasaidia wafungwa kujumuika tena katika jamii mara baada ya kuachiliwa huru. Mwisho wa Misa uwakilishi ulioongozwana Katibu,  Padre Siwa uliwatembelea wafungwa waliopo mahubusu huko Divo, kuelezea ukaribu wa Kanisa Katoliki kwa wafungwa. Walipewa vifaa vya chakula na bidhaa za usafi. Ikumbukwe kwamba ishara hii ya mshikamano imepanuliwa kwa magereza zote 34 zilizomo nchini Ivory Coast. Kwa mwaka wa kichungaji 2020-2021, kampeni ya kukusanya chakula ilitangazwa pia ili kurekebisha upungufu wa chakula katika magereza ya nchi hiyo yote.

17 April 2021, 15:34