Tafuta

maombi yanaendelea huko Haiti wakiomba kukombolewa waliotekwa nyara maombi yanaendelea huko Haiti wakiomba kukombolewa waliotekwa nyara 

Haiti:Makuhani,watawa na walei waliotekwa nyara huko wakombolewe!

Maombi bado yanaendelea kwa waamini wote huko Haiti ili wakombolwa waliotekwa nyara.Askofu mkuu ametoa wito maalum kwa mamlaka ya serikali ili kuhakikisha kuwa watu waliotekwa nyara wanaachiliwa haraka iwezekanavyo,bila kulipa fidia na nchi nzima iweze kupumua na kupata tena usalama na utulivu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Tunaomba usalama na amani kwa wamisionari wote na watu wote. Tunaomba kuachiliwa haraka na bila masharti kwa kaka na dada zetu waliotekwa nyara ”: Ndilo ombi la Askofu Mkuu Max Leroy Mesidor, wa Port-au-Prince, kuhusu utekaji nyara wa hivi karibuni tarehe 11 Aprili2021 ambapo watu 12 wakiwemo makuhani 7, watawa wawili, ndugu 3 wa kasisi, daktari na mhasibu. Padre na mtawa ni raia wa Ufaransa, na wengine ni Wahaiti.  Askofu mkuu ametoa wito maalum kwa mamlaka ya serikali ili kuhakikisha kuwa watu waliotekwa nyara wanaachiliwa haraka iwezekanavyo, bila kulipa fidia na nchi nzima iweze kupumua na kupata tena usalama na utulivu. Askofu mkuu Mesidor anaelezea ukaribu wake kwa watu wote ambao ni waathiriwa wa utekaji nyara na aina nyingine yoyote ya vurugu, mara nyingi kwa kutojali kwa mamlaka ya umma.

WAAMINI KATIKA SALA
WAAMINI KATIKA SALA

Makuhani, wachungaji, watawa wa kike na kiume wanajitoa kwa moyo wote katika  fungamani ya kibinadamu wa kaka na dada zao amethibitisha Askofu mkuu . Kwa njia hiyo wana haki, kama raia wengine wote, ya kuheshimiwa na usalama. Hawatakubali mbele ya vitisho . Askofu mkuu pia ametoa wito wa moja kwa moja kwa watekaji nyara na viongozi wao wa Krioli ya Haiti: Acheni kuharibu nchi, acheni kuharibu matumaini ya watu wa Haiti”. Baraza la  Maaskofu wa Ufaransa na Baraza la Watawa  wa kike na kiume nchini  Ufaransa wanaelezea wasiwasi mkubwa juu ya utekaji nyara wa watu saba nchini Haiti na waombea watekaji waachilie wanaume na wanawake wa amani waliowateka nyara na wasiongeze chuki zaidi ambapo umaskini na ukosefu wa usalama tayari vipo ”. Ni katika taarifa yao iliyochapishwa asubuhi tarehe 12 Aprili 2021 na maaskofu na watawa hao baada ya habari hizo za utekaji nyara huko Haiti.

WAAMINI WANASALI KADIRI WAWEZAVYO KWA UCHUNGU
WAAMINI WANASALI KADIRI WAWEZAVYO KWA UCHUNGU

Walietekwa nyara walikuwa wanakwenda kwenye sherehe za kusimimkwa kwa Paroko mmoja katika Parokia. Kwa mujibu wa Msemaji wa Baraza la Maaskofu wa Haiti wateka nyara wanataka Dola Milioni moja. Jumuiya ya Mapadre wa Mtakatifu -Jacques, iliyoko Guiclan (Uingereza), imeripoti kuwa makuhani wanne kati ya waliotekwa nyara ni washiriki wa jamii yao. Miongoni mwao, ni Wahaiti watatu (Padre Joseph Evens, Padre Jean Nicaisse Milien na Padre Joël Thomas) na Mfaransa (Padre Michel Briand). Padri wa tano, Padri Hugues Baptiste, ni kuhani wa Jimbo kuu la Cap Haitien. Mmoja wa sr hao wawili, Sr Anne-Marie Dorcélus, ni wa kundi Shirika la Masista Wadogo wa Mtakatifu Thérèse huko Port-au-Prince,  Padre wa tano ni Padre Hugues Baptiste, kuhani wa Jimbo kuu la Cap Haitien.

NJIA NI KUKIMBILIA MSALABA WA YESU
NJIA NI KUKIMBILIA MSALABA WA YESU

Mtawa wa Ufaransa, Agnès Bordeau, ni mtawa wa Wilaya ya Pommeraye na kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mapadre wa Mtakatifu Jacques wa wito wa kike wa kimisionari nchini Haiti. Umasikini mkubwa wa nchi hiyo ni pamoja na mizozo ya kisiasa ambayo imeongeza ukosefu wa usalama, ambao tayari umeenea sana kwa miaka mingi. Kanisa la Ufaransa lina ukaribu fulani na Kanisa la Haiti na kwa nchi hiyo yote. Katika wakati huu wa uchungu kwa ndugu na dada zao waliotekwa nyara, wanataka kuwahakikishia Wakatoliki wa Haiti na wakazi wake wote msaada wao na sala zao.

13 April 2021, 14:17