COMECE NA CEC COMECE NA CEC 

Cec na Comece:Pasaka ni tumaini katika kipindi cha janga Covid

Baraza la Makanisa Ulaya na Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya kwa pamoja wameandika ujumbe wao katika fursa ya siku kuu ya Pasaka,wakionesha matumaini ya ufufuko wa kuanza maisha mapya hasa katika kipindi cha Covid-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Matumaini ndiyo kiini cha ujumbe uliotangazwa na Baraza la Makanisa ya Ulaya (Cec) pamoja na Tume ya shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya ya Ulaya (Comece) katika fursa ya Siku kuu ya Pasaka ambayo mwaka huu itaadhimishwa Dominika, tarehe 4 Aprili 2021. Matumaini safi katika Ufufuko wa Kristo wakati wa janga la Covid-19, ndiyo kwa nja hiyo nguvu ya fadhila ya kitaalimungna ambayo imekumbushwa katika Hati hiyo, iliyoelekezwa zaidi ya yote kwa maskini na walio hatarini zaidi na iliyosainiwa na marais wa miili hiyo miwili, Mchungaji Christian Krieger na Kardinali Jean-Claude Hollerich.

Safari ya ukombozi kutoka utumwani

Pasaka inatukumbusha safari ya watu waliochaguliwa na Mungu kutoka utumwani, kutoka katika uonevu na kukata tamaa huko Misri, hadi ukombozi, furaha na matumaini katika nchi ya ahadi. Siku kuu hii inasherehekea hatua ya Kristo kutoka kukataliwa, kutelekezwa na  wanafunzi wake wa karibu, udhalilishaji, kutoka katika mapenzi na kifo tangu siku ya  Ijumaa Kuu, hadi kufikia maisha, furaha na ushindi siku ya Jumapili ya Pasaka, wanaandika  viongozi hao.

Uzoefu wa wagonjwa, vifo karantini kutokana na Covid-19

Mchakato wa njia hiyo kutokana na kukata tamaa hadi kufikia furaha, kutoka katika kifo hadi uzima, inajumuisha kuvuka shida, mashaka, mateso na uchungu, wanabainisha viongozi hawa wa makanisa. Hali inayofanana na uzoefi wa sasa wa ulimwengu wote kwa sababu ya janga la covid-19, wanasisitiza katika ujumbe huo wa pamoja CEC na COMECE. Kuishi karantini karibu mwaka mzima, kufanya uzoefu wa magonjwa na wasiwasi, kushuhudia huzuni na upotezaji wa watu wapendwa ina maana kubwa ya kufikia ujumbe wa Ufufuko katika Pasaka hii. Wakristo wa Ulaya, wanapitia sasa,  shukrani kwa namna ya pekee  kampeni za chanjo, kutoka katika kujitenga, kupoteza watu na wasiwasi hadi kupona, ili kurudia maisha mapya, ambapo kifo kwa hakika kinamezwa kwa ushindi (1 Wakorintho 15:54), wanaandika viongozi hao.

Tumaini la Yule Mfufuka litusaidie wakati wa janga la Covid-19

Hata hivyo  katika ujumbe huo wanaandika kuwa:“zawadi ya maisha mapya na uwezekano wa kuipokea na kuiishi lazima ibadilishe kabisa mtazamo ambao mtu anao juu ya hali halisi ya ulimwengu, pamoja na ugonjwa na kifo. Shukrani kwa Ufufuko, kiukweli, maovu na mauti ya mwili hayana neno la mwisho tena, kwa sababu maisha yetu katika Kristo yana utajiri wa matumaini na furaha ya milele”. Ujumbe wao wa  pamoja unahitimisha kwa matashi mema kwamba: “Tumaini la Yule Mfufuka litusaidie wakati wa janga la Covid-19”.

01 April 2021, 14:18