2021.04.21 Ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya Video kwa viongozi wa Nchi na serikali 2021.04.21 Ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya Video kwa viongozi wa Nchi na serikali  

Amerika Kusini:Celam yaunga mkono Ujumbe wa Papa kwa wakuu wa nchi

Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Amerika ya Kusini(Celam)wanaunga mkono ujumbe wa Papa Francisko alioutuma kwa washiriki wa Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Marekani uliofanyika Andorra.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tunaungana pamoja na wito wa Baba Mtakatifu kwa kutafakari kwa kina juu ya udugu na mshikamano kati ya serikali na wazalendo wa Ibero- Marekani ili kwa pamoja na sera za umma na kwa vitendo thabiti na vyema, tunaweza kukabiliana na kushinda janga kwa mtazamo wa ulimwengu wa kidugu na wa mshikamano katika  nyumba yetu ya pamoja. Ndivyo Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Amerika ya Kusini (Celam) wamebainisha katika taarifa yao ya  tarehe 24 Aprili 2021  wakiunga mkono kwa dhati  wa  ujumbe wa Papa Francisko alioutuma tarehe 21 Aprili,  kwa washiriki wa Mkutano wa 27 wa Ibero ya Marekani kwa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika kwenye ufalme wa Andorra.

Papa Francisko katika ujumbe huo aliwakumbusha watafakari juu ya shida za sasa ambazo ulimwengu unakatisha kwa sababu ya matokeo ya janga la Covid-19. Kwa mujibu wa taarifa ya maaskofu hawa, wanabainisha kwamba Baba Mtakatifu ameonesha wazi, mambo muhimu sana hasa la sadaka kubwa ambayo janga hili linadai kutoka kwa mataifa na raia wao, na alikumbusha kwamba sisi sote tumeathiriwa kwa njia moja au nyingine na kusisitiza umuhimu wa usambazaji wa chanjo kwa usawa wa wote.

Kwa kuungana na wito wa Papa, kwa maana hiyo, Shirikisho Celam limebainisha dharura ya kuwa na matendo ya dhati na mshikamano, ambao unaongozwa na udugu na upendo wa kijamii, kwa namna ya kutafakari upya uchumi wenyewe. Papa anatukumbusha kwamba lazima tuondokane na janga hili tukiwa bora kwa kufikiria tena uchumi wenyewe, ambao unapaswa kuwahudumia watu na faida ya wote na juu ya yote anapendekeza hitaji la ukweli la  kuwa na mfano wa urejesho wa ujumuishaji na endelevu ili isiwe kwamba  ni maskini wanaolipa gharama kubwa zaidi ya majanga haya ambayo yanaathiri familia yetu ya wanadamu.

28 April 2021, 11:37