Pasaka imefika kwa ajili ya kusaidia kuupokea ujumbe wa kinabii wa Papa Francisko nchini Iraq, anasema Askofu Mkuu  Paul Desfarges katika ujumbe wake wa Pasaka 2021 Pasaka imefika kwa ajili ya kusaidia kuupokea ujumbe wa kinabii wa Papa Francisko nchini Iraq, anasema Askofu Mkuu Paul Desfarges katika ujumbe wake wa Pasaka 2021  

Algeria:Ask.Desfarges:Pasaka na Ramadhani viwe fursa ya kukuza udugu!

Katika fursa ya Siku Kuu ya Uufuko wa Bwana,Askofu Mkuu wa Algeria ameandika ujumbe wake kwa waamini wake akisema kuwa“Pasaka inafika kutukumbushakupokea ujumbe wa kinabii wa Papa Francisko nchini Iraq wakati wa hija yake mwezi mmoja uliopita”.Pasaka na Ramadhani ni fura ya kukuza udugu uliohimizwa na Papa hivi karibuni katika hija yake ya kitume nchini Iraq.

Na Sr. Angela. Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu wa Algeria, Paul Desfarges katika fursa ya Pasaka na Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambao utaanza tarehe 13 Aprili na kuhitimishwa manmo tarehe 12 Mai 2021, kuwa “Pasaka imefika kwa ajili ya kutusaidia kuupokea ujumbe wa kinabii wa Papa Francisko nchini Iraq, mwezi mmoja uliopita”. Kwa mujibu wa maelezo kutoka katika Tovuti ya Kanisa la Algeria, Askofu Mkuu anahimiza kwamba hawapaswi kusahau mchakato wa hija ya udugu wa nchi ya Ibrahimu na ujumbe wa matumaini ambayo alishuhudia.

“Pasaka inatuoenesha kuwa Mungu mwenyewe ni uhusiano wetu wa kidugu kwa wote. Kwa njia ya ufufuko wake, Yesu Kristo, ambaye alijifanya kaka wa wote anakuja kutusimulia uwepo wake katika moyo wa kila mtu” amesisitiza Askofu Mkuu wa Algeria Algeri. Askofu Mkuu Desfarges, aidha ameeleza kuwa “udugu ni ishara angavu ya upendo wa Mungu ambao uliingia katika moyo wa watu. Huku Uru nchini Iraq ambao ni mji asili wa Ibrahimu Baba Mtakatifu alituonesha Pasaka ya sasa kwa kwenda kukutana na ndugu wa madhehebu tofauti ya imani ya kiislam, ya tamaduni ya kiishia na kisuni  na aina nyingine ndogo kama yazidi, mazdei, sabei na nyingine”, amefafanua Askofu Mkuu.

Aliweza kukutana na  kiongozi mkuu wa kiroho Ayatollah Al-Sistani kwa mara ya kwanza kama ndugu, yaani ndugu mwamini. Askofu Mkuu wa Algeria aidha amekumbuka kuwa “zaidi kuwa huko Uru, Baba Mtakatifu Francisko aliwakabidhi ujumbe wa udugu na kuthibitisha kuwa Aliye juu anatualika tusitengene kamwe kama jinsi ambavyo yeye yuko karibu nasi” na ambaye mbali na Mungu, ni kuhimiza ndugu mwingine ambaye ni uzao wa Ibarahimu na wanawakilishi wa dini nyingine kwa kuisi na jukumu hili la kusaidia kaka na dada kuinua mtazamo na sala kwa Mungu. Mwaliko wa Papa kwa dini zote ni kufanya kazi naye kwa ajili ya amani akiweka wazi na kwamba huu ndiyo wito wa Kanisa la Algeria. Yaani kufanya kazi kwa ajili ya amani huku wakijikita kudumisha udugu kwa wote.  Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Desfarges anasema kipiid muafa kwa ajili ya kuishi udugu itakiwa pia Ramadhani ambayo itaanza hivi karibuni.

Kipindi hiki cha upyaisho wa kiroho kwa ajili ya ndugu zetu kaka na dada waislam ni fursa ya kuunganisha kwa moyo na sala zao na hata kuishi vipindi vya nguvu ya maisha kidugu kwa mfano, wakati wa chakula cha usiku kuwaalika wengine. Na pia mwaka huu unatoa jaribu familia nyingi na hivyo mfungo wa Ramadhani utakuwa kwa dhati kipinid muafaka cha mshikamano mkuu.

03 April 2021, 16:00