MAASKO WA IMBISA MAASKO WA IMBISA 

Wito wa Imbisa kwa Cabo Delgado:Dharura ya kakabiliana na ukosefu wa usawa

Wito wa Shirikisho la Mabaraza ya Kanda ya Kusini mwa Afrika Imbisa wanasema ipo dharura ya kukabiliana na ukosefu wa usawa kiuchumi na kijamii kwa namna ya pekee kwa vijana.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Maaskofu wa Afrika ya Kusini wanafuatilia kwa wasiwasi mkubwa juu ya janga la maendeleo ya hali halisi ya Mkoa wa Cabo Delgado, nchini Msumbiji, mahali ambapo mashambulio ya kigaidi ya vikundi vinavyohusiana na Dola la Kiislamu yanaendelea kuongezeka kwa wahanga na wamehama makazi yao zaidi ya nusu milioni. Kitovu cha mapigano katika wiki za hivi karibuni kimekuwa mji wa Palma, eneo la mashambulio ya kinyama zaidi na wanamgambo wa kijihadi. Katika taarifa iliyotolewa tarehe 27 Aprili 2021, Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Kusini mwa Afrika (IMBISA), ambayo inawaleta pamoja maaskofu wa Angola, Botswana, Eswatini, Lesotho, Msumbiji, Namibia, São Tomé na Principe, Afrika Kusini na Zimbabwe, inaangazia hasa juu ya hali ya vijana, walio hatarini zaidi pia katika matokeo ya janga la Covid-19. Kwa sababu ya vizuizi vilivyowekwa na dharura ya kiafya, vijana wengi kwa hakika wametumia muda mrefu bila kuweza kwenda shule. Mafunzo ya umbali ambayo maskini hawawezi kuyapata, yameangazia zaidi tofauti kubwa za kiuchumi na kijamii ambazo nchi zote za kusini mwa Afrika zinakabiliwa nazo.

Katika taarifa hiyo iliyotiwa saini na rais wa Imbisa, Askofu Lucio Andrice Muandula inathibitisha kuwa shida ya ukosefu wa usawa, hasa ile ya uchumi imewaacha vijana wengi wakiwa wazi hasa katika suala la unyonyaji wa wale ambao wanaochochea vurugu na maovu mengine ya kijamii.  Pia inalazimisha wengi wao kuhama ili kupata riziki mahali pengine. Hali hii inakwaza na kukosea heshima ya mwanadamu na hasa haki ya utakatifu wa kuishi na ile ya watu kuishi kwa amani katika nchi yao wenyewe, maaskofu wa kusini mwa Afrika wamebainisha. Katika sura hii ya kutatanisha kwa hakika, lakini maaskofu wanaona hata maendeleo chanya. Hasa, wanapongeza tamko la hivi karibuni la Baraza la Maaskofu wa Msumbiji (Cem) ambalo lililaani vikali vurugu ya huko Cabo Delgado, pia wakinyooshea kidole vikundi vya vyenye kutafuta mafao ambao wanataka kuchukua rasilimali za mahalia, lakini pia juhudi za Kanisa na taasisi nyingine kuleta misaada kwa waathiriwa. Aidha wamebainisha kutiwa moyo na juhudi zinazofanywa na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) ili kupata suluhisho la kudumu kwa shida za eneo hilo.

Kwa upande wa maaskofu wa kusini mwa Afrika, hata hivyo, wanasema hata hivyo hiyo yote haitoshi. Kwa maana hiyo ndipo wametoa wito kwanza kabisa kwa Sadc yenyewe na kwa Jumuiya ya Afrika ili kufanya zaidi kusuluhisha mgogoro wa Cabo Delgado. Imbisa pia amegeukia serikali ya Msumbiji ikiomba sio tu kuepusha juhudi zake ili kuhusisha jumuiya ya kimataifa dhidi ya vurugu, ambayo imegharimu upotezaji wa maisha ya wanadamu lakini pia rasilimali muhimu ya kujikimu kwa idadi ya watu. Hatimaye ombi kwa serikali zote katika kanda wa kufikiria tena mifumo yao ya kiuchumi ambayo hairuhusu kushinda tofauti zilizomo za ukosefu wa usawa kijamii, kwa kuzingatia kipaumbele cha vijana ambao wanasema lazima wawe katikati ya maendeleo ya uchumi katika nchi hizi. Wakinukuu maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wa ‘Fratelli tutti’, yaani ‘Wote ni Ndugu’, tamko hilo la maaskofu linahitimishwa na mwaliko kwa Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kutafuta na kutembea pamoja kwa amani kama Mtakatifu Francis wa Assisi na kuota ndoto ya jinsi mtu mmoja wa familia ya wanadamu na kama watoto wa ardhi moja ambayo ni nyumba yao ya pamoja ya kuishi.

30 April 2021, 13:22