Taadhari inapaswa kuchukuliwa nchini Tanzania dhidi ya virusi vya Corona au COVID-19 Taadhari inapaswa kuchukuliwa nchini Tanzania dhidi ya virusi vya Corona au COVID-19 

Tanzania:Tahadhari inahitajika kwani waathirika wa Janga la Covid-19 wa Kanisa waongezeka

Nchi yetu sio kisiwa.Lazima tujilinde,tuchukue tahadhari na tuombe Mungu kwa nguvu zetu zote ili janga hili lisitufikie,ni wito uliokuwa umetolewa na kiongozi wa Kanisa nchini Tanzania,ambapo hivi karibuni,Msemaji wa Tec amerudia kuhimiza waamini na wenye mapenzi mema kuwa na tahadhari kutokana na vifo zaidi ya mapadre 25 na idadi kubwa ya watawa, manesi na madaktari wa kikatoliki vilivyokea karibu miezi miwili.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Kwa miaka miezi miwili zaidi ya mapadre 25 na watawa na manesi katoliki na madaktari karibu 60 wamefariki dunia kutokana na matatizo ya upumuaji. Amesema hayo Padre Charles Kitima, Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).  "Jambo hili halijawahi kutokea kwa kipindi kifupi namna hiyo amesema".  Ni katika muktadha wa hali halisi ya janga la virusi vya corona vinavyo endelea kuyumbisha ulimwengu wote  ambapo Padre Kitima anatambua wazi kwamba waliokufa hawezi kweli wote kuwa ni kutokana na  Covid-19 lakini kutokana na dalili za gonjwa hilo na uzoefu wa vifo vya namna hiyo.  “Sisi kama Kanisa hatuna vipimo na madkatari hawawezi kusema kwa sababu hawana ruhusa ya kufanya vipimo hivyo”.

FR KITIMA KATIBU WA TEC KUWA NA TAHADHARI YA COVID

Hadi sasa  mamlaka ya Tanzania haikusasisha data za Covid-19  tangu mwezi Mei mwaka jana ambapo idadi ya kesi iliyokuwa imethibitishwa ilikuwa 509 na waathirika 21. Licha ya sera za kisiasa  kukana uwepo wa virusi nchini na viongozi wa eneo hilo, Padre Kitima ameomba kila mtu kwa hisia ya uwajibikaji: “virusi vya vipo”. Tunawaomba  mchukua tahadhari. Tunahitaji kuongeza juhudi zetu kujilinda. Tuna jukumu la kulinda wazee na watu wenye afya mbaya kwa kuchukua tahadhari zinazohitajika. "Watanzania wana haki ya kupokea habari sahihi za kisayansi juu ya Covid-19 kwa sababu ukosefu wa habari halisi juu ya virusi inaeneza hofu na mkanganyiko kati ya watu”, ameomba suala hili.

Mnamo Februari, Rais wa  Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu Gervais Nyaisonga, wa Jimbo Kuu la  Mbeya, aliwahimiza watanzania wasiwe watumwa wa woga, lakini wafuate ushauri wa wataalam: “Watanzania, tunahimizwa kutokuwa na utumwa wa woga. Hofu ni silaha inayoweza kumdhoofisha mtu”.

Mwisho wa mwezi Januari maaskofu kadhaa mahalia nchini Tanzania , waikuwa tayari wameweka taahadahri kwa waamini juu ya ( wimbi jipya la virusi vya corona , na ambavyo vimesababaisha ongezeko la vifo. (taz. Fides 29/1/2021). “Nchi yetu sio kisiwa ... Lazima tujilinde, tuchukue tahadhari na tuombe kwa Mungu kwa nguvu zetu zote ili janga hili lisitufikie”, alikuwa amesema kiongozi huyo.

06 March 2021, 15:56