KOZI YA ULINZI NA USALAMA NCHINI SUDANI KUSINI KOZI YA ULINZI NA USALAMA NCHINI SUDANI KUSINI 

Sudan Kusini,Askofu wa Tombura-Yambio:Msamaha ni njia pekee ya amani!

Askofu Edward Hiiboro Kussala amezindua wito kwa ajili ya amani kitaifa katika nchi yote ambayo inaendelea kuona machafuko na mauaji huku akihimiza kwamba inahitajika kuwafanya waelewe kwatu uwa vurugu siyo njia ya kusuluhisha migogoro.Kanisa liko mstari wa mbele na viongozi wa madhehebu mengine kuzungumza na serikali.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Wanafika katika vijiji na miji wakiwa na bunduki na bastola, wanashambulia, wanaiba na kuua. Nao hukimbia bila ya hata kuacha alama. Sudan Kusini inakabiliwa na ongezeko kubwa la vurugu ambazo hazijawahi kutokea. Kulingana na takwimu za hivi punde zilizotolewa na Tume ya Haki za Binadamu ya nchi hiyo ya Afrika asilimia 75 ya taifa hilo limetikiswa na mashambulio ya kikatili, hasa katika ngazi za mitaa mahalia. Na matukio ya vikundi vya roho mbaya, ambavyo hushambulia bila kuadhibiwa mbele ya haki, ni wasiwasi juu ya kuongezeka kwa nguvu: kwa mwezi mmoja tu, makumi ya watu wasio na hatia wameuawa. Ndivy Askofu wa Jimbo la Tombura-Yambio, Edward Hiiboro Kussala, anasimulia kwamba nyumba na tukio hilo la  mauaji kuna shauku kubwa ya kutaka kuona linamalizika, hasa kwa kupitisha mamlaka na sheria, ambayo zaidi ndiyo inaongeza umaskini sugu hasa kwa vijana wengi. Mkananyiko huo mbaya ndiyo umesababisha Askofu huyo kuzindua, hasa katika kipindi hiki cha nguvu cha Kwaresima wito kwa ajilli ya amani na kuomba msamaha.

Kwa mujibu wa Askofu Kusala anasema: “Nimewaalika watu wetu kuwa watulivu na wasitumie vurugu. Niliwahakikishia ukaribu wangu kwa familia zilizofiwa na kwa wale wote ambao wameshtuka na kuogopa”, Amesisitiza Askofu ambaye  kulingana na suala la  kusamehe, katika nchi hiyo iliyojaribiwa na maumivu, haiwezekani, kiukweli labda ndiyo inabaki kuwa njia pekee ya kupata utulivu: “Tunahitaji kuzungumza na watu, kuwafanya waelewe kuwa kupitia njia ya vurugu hakusuluhishi shida, badaka yake kunahitaji kutafuta njia ya  halali ya kuleta amani na zaidi suala la wahalifu ambao hawafikishwi mahakamani kwa sababu kwamba  yule ambaye angefany hivyo  anaogopa matokeo ya  vurugu. Lakini ikiwa tunataka Sudan Kusini yenye amani na mafanikio lazima tujisamehe, kama Injili na Kanisa inavyofundisha”.

Lengo la amani ya kijamii na upatanisho sio rahisi, lakini Kanisa halibaki nyumba kwani Maaskofu wanafanya mazungumzo ya karibu na serikali ya umoja wa kitaifa. Askofu Mkuu Kussala ameelezea kwa undani kuwa Kanisa linakutana na viongozi wote wa chama wakiomba wafanye kazi pamoja kwa faida ya watu wote. Pamoja nao pia wanashughulikia shida ya vurugu za kikabila. Lakini, kwa bahati mbaya, ni mchakato wenye vikwazo kwa sababu kuna ufisadi mwingi na Kanisa mara nyingi halisikilizwi. Operesheni ya mazungumzo ambayo pia hufanywa kwa msaada wa muungano wa madhehebu mengine ya kidini. Askofu wa Tombura-Yambio ndiye rais wa kikundi cha kidini ambacho kimekuwa kikijaribu kwa muda kutafuta namna ya kuwaokoa waathiriwa na wauaji kutoka kwa vurugu, kwa maana hiyo amesema kazi yao ni kuhakikisha inazaa matunza mengi na mazuri. Hii ni njia sahihi inayostahili kuendeleza”.

31 March 2021, 12:58