2021.03.02 Misa katika madhabahu ya Mama wa Kibeho,Rwanda 2021.03.02 Misa katika madhabahu ya Mama wa Kibeho,Rwanda 

Sala kwa ajili ya ziara ya Papa yaandaliwa na Radio Maria Afrika,Ufaransa&Uswizi

Katika fursa ya maadhimisho miaka 30 tangu Mama Maria wa Kibeho nchini Rwanda alipowatokea kijana Marie Claire tarehe 2 Machi 1981.Radio Maria Afrika,Radio Maria Ufaransa na Uswizi wanaungana kwa pamoja kusali kwa ajili ya ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Iraq.Misa itaadhimisha Machi 2 saa 11:00 jioni katika Madhabahu ya Mama Maria huko Kibeho Rwanda.

 

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 2 Machi 2021 saa 11.00 jioni masaa ya Ulaya, Radio Maria Afrika, Radio Maria Ufaransa, na Uswizi wataungana pamoja kusali kwa ajili ya ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Iraq, inayotarajiwa kuanza Ijumaa, tarehe 5 hadi 8 Machi 2021. Tukio la maombi linafanyika katika maadhimisho ya Misa takatifu iliyoandaliwa kufanyika katika  Madhabahu ya Mama Maria wa Kibeho nchini Rwanda, katika fursa ya kumbu kumbu ya Miaka 30 tangu Mama wa Kibeho alipomtokea kijana Marie Claire Mukangango na wenzake wawili baadaye mnamo 1981. Marie Claire aliyemwona mama Maria anajulikana sana kwa ujumbe aliopewa kuutangaza kuhusu kusali Rozari ya mateso Saba ya Bikira Maria ambayo inahusu wito wa haraka wa kufanya toba: “Tubuni, tubuni, tubuni! Ongokeni wakati muda bado upo".

MADHABAHU YA MAMA WA KIBEHO
MADHABAHU YA MAMA WA KIBEHO

Kwa mujibu wa Jean Paul Kayihura, Mwakilishi wa Radio Maria kwa upande wa Bara la Afrika, akizungumzia kuhusu kuombea ziara ya Papa amesema "katika tarehe hii kwa hakika ni kumbu kumbu nzuri ambayo imekuwa fursa kuandaa maombi kwa ajili ya ziara ya Papa ambayo inatamaniwa sana na watu nchini Iraq kama ilivyo hata ulimwengu mzima kuona nchi hiyo inakuwa na amani. Katika siku hii ya kumbu kumbu ya kutokea kwa Maria nchini Rwanda, ni fursa ya utume wa Radio Maria kuungana na waamini wote pia kusali kwa ajili ya Papa.  Tukio la kutokea kwa Bikira Maria wa Kibeho katika ardhi ya Afrika ilikuwa ni unabii na bado ni unabii unaondelea ndani ya Kanisa na kwa ulimwengu mzima”.

Ikiwa ni kweli kwamba kwa mama Maria kila roho na ulimwengu wote umeingiliana katika mpango mmoja wa mapenzi kwa wale wanaopenda kufuata nyayo za Maria kwenye njia ya ubinadamu wanajua ni ukweli kuwa ardhi ya Rwanda imebarikiwa na kujaa neema. Tukio la  matokeo ya Mama wa Kibeho yalianza mnamo 1981. Kwa maana hiyo matukio yasiyo ya kawaida kuhusu Rwanda yalidumu kwa miaka minane, kuanzia  tarehe 28 Novemba 1981 hadi 28 Novemba 1989, wakati ambapo Mama yetu aliwapa ujumbe wake wasichana watatu: Nathalie (18), Marie Claire (21) na Alphonsine (miaka 16). Moja ya ukweli wa kushangaza wa mzunguko huu wa maono ya Maria upo kwenye maono ambayo Mama Yetu anaonesha mfululizo kwa wasichana hao mnamo tarehe 15 Agosti 1982.  Hao waliona: Mito ya damu, moto unaowaka, watu wakiuana na shimo kubwa ambalo watu wengi karibu wanataka kuanguka ... wasichana waliona yote haya wakati Mama wa Neno alionekana kwao akiwa na huzuni kubwa na kulia.

WAKURUGENZI WA RADIO MARIA AFRIKA WAKIWA KIBEHO
WAKURUGENZI WA RADIO MARIA AFRIKA WAKIWA KIBEHO

Madhabahu inaitwa Mama wa huzuni. Ingawa ujumbe huo ni wenye nguvu lakini kisiasa siyo sahihi, hatupaswi kusahau kwamba Mama yetu wa huzuni, kama Madhabahu ya Kibeho inavyoitwa  pia ni Mama wa Tumaini. Mama anaonekana  na kusema ukweli kwa sababu anataka sisi wote tuokolewe, anataka twende wote mbinguni pamoja naye! Ndio maana tunapaswa kusikiliza na kutekeleza yale anayosema. Amesema hayo Padre Jean Claude ambaye alinusurika katika mauaji ya kimbari na ambaye mara nyingi ameishi uzoefu wa nguvu ya umama wa Maria, si tu wakati wa tukio la mauaji ya kimbari lakini katika maisha yake yote hasa tangu yeye awe kuhani wa Mungu.

02 March 2021, 10:32