Askofu Mkuu Tarcisius Isao Kikuchi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tokyo Askofu Mkuu Tarcisius Isao Kikuchi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tokyo 

Mshikamano wa Askofu Mkuu wa Tokyo kwa raia wa Myanmar

Askofu Mkuu Taciosius Isao Kikuchi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tokyo na Makardinali 12 wa Asia wanaonesha mshikamano wa Kanisa la Myanmar kufuatia na kuendelea kwa vurugu na machafuko nchini humo baaada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyokea mnamo Mosi Januari iliyopita.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Maneno ya mshikamano kutoka Makanisa ya Asia kwa ajili ya watu wanaoteswa wa Myanmar hayaishi, wakati  ukandamizaji  na umwagaji damu kwa maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi yalitokea manmo 1 Februari iliyopita unaendelea. Kwa hakika habari zilizotolewa zinathibitisha kuwa watu kama  91, kwa mfano tarehe 27 Machi walikufa na ambayo ilikuwa ni idadi kubwa zaidi ya kila siku kuwahi kurekodiwa na mapinduzi hayo. Katika barua iliyotumwa siku za hivi karibuni kwa Baraza Maakofu  wa  Myanmar na kwa Kardinali Charles Maung Bo, askofu mkuu Isao Kikuchi, wa Jimbo Kuu Katoliki la Tokyo, ametaka kuonesha ukaribu hasa katika sala ya Jimbo kuu kwa ajili ya Kanisa dada la Myanmar.

Katika barua hiyo inabainisha kwamba  kwa wakati huu wa Kwaresima, wanaomba kila mmoja ajaribu kupyaisha majitoleo yao kwa Kristo na kujitahidi kuishi maisha mapya katika jumuiya yao.  Askofu anaomba kwamba sadaka na maombi ya watu wa Myanmar yalete amani na upya kwa nchi hiyo. Barua hiyo inaonesha wasiwasi mkubwa juu ya hali ya sasa na athari inayotokea kwa  watu. Askofu Mkuu Kikuchi  anawahakikishia mshikamano wake kwa Kanisa la Myanmar, wanaojikita kuhudumia wanyonge na kuhamasisha amani kwa wote

Askofu Mkuu kwa aidha amesema: “Pamoja na Baba Mtakatifu tunaomba kwamba wale walio na mamlaka wafanye kazi kwa ajili ya mapenzi ya dhati kutumikia haki ya wote na msingi wa haki za binadamu na kiraia, kuhamasisha  haki na utulivu wa kitaifa kwa mshikamano, kidemokrasia na amani”. Katika barua hiyo  pia inaendelea huku ikinukuu hotuba ya hivi karibuni na Askofu Mkuu Ivan Jurkovic, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa mataifa huko Geneva.

Kwa njia hiyo pia Askofu mkuu wa Tokyo anakumbuka ziara yake huko Myanmar, mnamo Februari 2020, wakati alipata fursa ya kujua hali halisi ya Kanisa huko Myanmar, na kwa kushangazwa na imani kubwa ya Wakatoliki wa Birimania. Matumaini ya kiongozi huyo ni kwamba "matumaini na matarajio yao hayaangamizwi." Askofu Mkuu Kikuchi anahitimisha kwa maneno ya Kardinali Bo: “Amani inawezekana, amani ndiyo njia pekee", na anawakikishia maombi yake kwa jumuiya nzima ya Wakatoliki kutoka Tokyo kwa ajili ya Myanmar.

Kwa kuongezea zaidi barua ya askofu mkuu wa Tokyo inatoa wito kwa mara nyingine ambao tayari umekwsha tuolewa na mshikamano katika wiki za hivi karibuni na Makanisa barani Asia na Kanisa na watu wa Birimania. Miongoni mwa miito hiyo ni barua ya wazi iliyochapishwa siku za hivi karibuni na makadinali 12 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Asia (Fabc) kwenda kwa Kardinali Charles Bo, ambapo wanaelezea kuunga mkono kwao kwa kujitoa kwa Kanisa la Birmania  ili kupata suluhisho la amani katika mzozo na dhidi ya vurugu za kijeshi mbele ya raia wote wasio na hatia.

Katika ujumbe huo, makadinali barani Asia waliwageukia wanajeshi, waandamanaji na watendaji wote wa kisiasa wa Birimania, wakisisitiza, pamoja na Kardinali Bo, kwamba "vurugu kamwe sio suluhisho; nguvu kamwe sio suluhisho. Inaongeza maumivu tu na mateso zaidi, vurugu zaidi na uharibifu”. Waliweza kukumbusha kuwa "Asia ni bara la amani na matumaini, na ni familia moja". Barua hiyo ilihitimishwa kwa kurudia tena kwamba amani inawezekana.

29 March 2021, 12:39