KARDINALI SAKO ALIAMBATANA NA PAPA KILA ENEO LA ZIARA YAKE KARDINALI SAKO ALIAMBATANA NA PAPA KILA ENEO LA ZIARA YAKE 

Kard.Sako:Ziara ya Papa inaweza kubadili Iraq

Umekuwa wakati maalum kwa ajili ya nchi yetu ambayo ni matarajio baada ya ziara hii inawezekana kuona mabadiliko zaidi.Ndiyo maoni ya kwanza yaliyotolewa na Patriaki wa Babilonia ya Kikaldayo Kardinali Louis Raphaël I Sako,mara baada ya Papa Fracisko kuondoka nchini Iraq.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amerudi mjini Vatican tarehe 8 Machi 2020 kutoka Iraq. Kwa watu wengi wameifikiria safari yake ni ya kihistoria ambapo miongoni mwao  ni Shirikisho la Mabaraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini (CELAM). Katika ujumbe wao, Maaskofu hao wanaelezea shukrani zao kwa Papa Francisko kwa  kufanya ziara hiyo katika Nchi ambayo inaishi jumuiya ndogo katoliki na inayoteseka. Celam inaonesha ukaribu wake na kusali  ili ziara yake ya kichungaji aliyohitimisha katika muktadha wa janga la Covid-19, na ambalo linaendelea kuumiza ulimwengu mzima, iweze kuleta matunda. Maaskofu wanabainisha katika ujumbe huo kwamba imekuwa ziara ya kutunza ustaarabu ambao unaonesha ishara ya Baba yetu Ibrahimu ambaye anaunganisha Wakristo, Wayahudi na Waislamu na kufanya kuwa wajumbe wa familia moja ya kibinadamu.

PAPA AKIWASLIMU WATOTOT
PAPA AKIWASLIMU WATOTOT

Huu ni ushuhuda wa ujasiri uliooneshwa na Baba yetu mpendwa Papa Francisko, kwa kutembelea wale ambao wanateseka kutokana na matokeo ya itikadi kali za kidini na hadi kufikia kufikadini wamesisitiza maaskofu hao. Papa Francisko alijiwakilisha kwao kama mwanahija wa kidugu ulimwenguni na ziara yake itakuwa chmbo ambacho bilashaka kitawatia moyo na kuwaimarisha imani katika Kanisa hili linaliteseka. Ziara hii ya Papa nchini Iraq , itakuwa sehemu ya matukio muhimu zaidi ya hitostia na itabiki imesikikwa ndani ya mioyo ya ndugu zetu wairaw ambao hawatasahau kamwe kuwa Baba Mtakatifu mwenyewe alikwenda katikati yao”.

PAPA AKIWA KATIKA MKUTANO
PAPA AKIWA KATIKA MKUTANO

Matumaini ya Celam lakini pia uhakika ni kwamba safari hyo itaweza kusaidia kushinda chuki na vurugu , kwa kuhamasiaha zaidi heshima ya utakatifu wa maisha. Wanamshukuru tena Papa kwa ajili ya ushuhuda wake wa ukaribu na wale ambao wanakabiliana na matokeo ya vita, kuteswa na matatizo. Ujumbe wa Celam unahitimishwa kwa mwaliko wa Maaskofu wote wa Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribie ili kuendeleza uhamasishaji kati ya makuhani, watawa, na waamini waleo sala isiyo isha ambayo inamsinidkiza Mfuasi wa Petro ili ziara yake ya kitume nchini Iraq izae matunda mengi ya kichungaji na kuhamasisha zaidi mazungumzo ya kidini.

PAPA AKIAGWA
PAPA AKIAGWA
08 March 2021, 17:11