Shambulizi la kigaidi katika Kanisa Kuu la Makassar nchini Indonesia Shambulizi la kigaidi katika Kanisa Kuu la Makassar nchini Indonesia 

Indonesia:Waathirika wa shambulio la kigaidi

Shambulizi la kigaidi limetokea tarehe 28 machi 2021 mbele ye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu la Makassar,wilaya ya Kusini Mshariki mwa Sulawalesi,nchini Indonesia na kusababisha majeruhi wakati wamemaliza misa na wanakwenda nyumbani.Mshambulizi alifika na kusimama lango la pembeni mwa Kanisa Kuu akiwa na pikipiki na kujilipua.Papa amesali kwa ajili ya waathirika wa tukio hilo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Inasadikika watu 14 wamejeruhiwa na kifo cha mtu mmoja wakati wa shambulio la kigaidi lililotokea asubuhi tarehe 28 Machi 2021, mbele yeaKanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu la Makassar, wilaya ya Kusini Mshariki mwa Sulawalesi, nchini  Indonesia. Mwisho wa tafakari ya Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, na mara baada ya kuhitimisha Misa ya Dominika ya Matawi amewakumbuka waathirika wa vurugu kwa namna ya pekee wa tukio hilo na kusema: “Tusali kwa ajili ya waathiriwa wote wa vurugu kwa namna ya pekee kwa wale ambao wameaathirika katika shambulio lililotokea leo hii asubuhi nchini Indonesia mbele ya Kanisa Kuu la Makassar. Mama Maria atusaidie na ambaye anatutangulia katika njia zetu za imani”.

Kwa mujibu wa Polisi mahalia shambulio hilo lililotokea majira ya saa 3:20 asubuhi wakati ilipokaribia pikipiki katika lango la pembeni mwa jengo baada ya misa ya Dominika ya Matawi na watu wakiwa wanarudi nyumbani kwao. Hata hivyo taarifa inabainisha kwamba ingekuwa mbaya sana iwapo pasingekuwapo na maaskari walinzi mbele ya Kanisa Kuu hilo. Na aliyefanya hivyo amekufa kwa mujibu wa Padre Wilhelmus Tulak kwa waandishi wa habari.

Hii siyo mara ya kwanza makanisa nchini Indonesia kusongwa na makundi haya ya kijitahadi nchini, ambapo sehemu kubwa ya watu ni waislamu zaidi ulimwenguni. Ilikuwa maamo Mei 2018 watu sita wa familia moja walijitoa kufa katika makanisa matatu, moja la kikatoliki na mawili ya kiprotestanti huko Surabaya, mji wa pili wa nchi na kuwawa waamini wengi . Familia hiyo ilikuwa ni mmoja wa kikundi cha kijhadi cha Jamaah Ansharut Daulah (Jad).

29 March 2021, 09:34