Patriaki Sako azungumza juu ya maandalizi ya ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Patriaki Sako azungumza juu ya maandalizi ya ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini 

Hija ya kitume Papa Francisko nchini Iraq:Ziara yake ni kwa ajili ya wote!

Wakristo hata Waislam wametunga nyimbo kwa ajili ya kumkaribisha Papa.Ni lazima kusema kwa nguvu,Papa anakuja na hakuna hofu,wala kwa ajili yake hata kwa watu wa Iraq.Ziara hii ni kama ndoto ambayo inakuwa halisi.Sisi ni kama watoto wadogo ambao wanaandaa siku kuu.Kuanzia kwa mkubwa hadi mdogo zaidi yetu.Amesema hayo Patriaki Sako akisistiza kuwa Papa anakwenda kwa ajili ya wote na wafiadini ni utukufu wao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kabla ya mkesha wa ziara ya Papa Francisko nchini Iraq, ambayo inatarajiwaa kuwanzia Ijumaa tarehe 5 hadi 8 Machi 2021, Kardinali Luis Raphael Sako, Patriaki wa  Babilonia ya Wakaldayo amefafanua maandalizi na shauku kubwa iliyopo katika nchi hiyo  kwa Shirika la habari za Kimisionari FIDES na juu ya matumaini ya nguvu ya jumuiya na watu ambao wanasubiri kufika kwa Askofu wa Roma, na kama fursa ya kugundua kwa upya thamani binafsi na kutazama kwa matumaini na shukrani za wakati ujao. Patriaki amesema “Nimerudi sasa hivi kutoka Kanisa Kuu mahali nilipokuwa nimekwenda kuona maandalizi. Pale nimemkuta mwanamke mmoja, mbele ya groto ya Mama Maria. Mwanamke mwislam alikuwa amekuja kusali kwa Bikira Maria. Yeye amesema “ asante Mungu kwa kuwa Papa anakuja. Na ujio wake ni kama matumaini ya mwisho kwa wairaq”. Kardinali ameongeza,  “kuna shauku maalum ambayo inawagusa wote”. Na  mara nyingi amesisitiza Kardinali kuwa utafikiri karibu waislam wanayo furaha kubwa zaidi kuliko wakristo… “Sisi tumepamba makanisa yetu, lakini watu wa Iraq wote wamepamba mji wao…Kuna bendera za Vatican na mabango mbalimbali ya kukaribisha kila sehemu hata Najaf na Nassiriya…na  hata  Mosul, mji ambao unawakilisha kwa mara nyingine majereha yote”. Kardinali Sako amesisitiza!

Nyimbo  za kiislam kwa ajili ya Papa

Kardinali Sako akiendelea amesema “Waislam wametunga nyimbo kwa ajili ya kumkaribisha Papa. Ni lazima kusema kwa nguvu, Papa anakuja na hakuna hofu, wala kwa ajili yake na wala kwa watu wa Iraq. Ziara hii ni kama ndoto ambayo inakuwa halisi.  Sisi ni kama watoto wadogo ambao wanaandaa siku kuu. Kuanzia kwa mkubwa hadi kwa ndogo zaidi yetu”. Patriaki amesisitiza juu ya sentensi za Ayatollah Alì wa Sistani zilizoandikwa katika mabango ya matangazao kwenye picha ya mamlaka kuu ya Waashia katika Nchi iliyo karibu na ile ya Papa Francisko:  “Al Sistani amesema: Ninyi ni sehemu yetu, na sisi ni sehemu yenu’. Hii ni namna ya kuonesha kwamba sisi sote ni ndugu”, kiongozi wa kikaldayo amesisitiza.

Papa anataka kuwatia moyo na matumaini ya kuvumilia

Patriaki wa Kanisa la Wakaldayo pia amefunua uwanja tafsiri nyingi zilizotolewa za safari ya papa ambayo anaona kuwa tafsiri hizi ni kupotosha, kuanzia na wale ambao wanasisitiza ziara hiyo ya kitume kama operesheni inayolenga kuimarisha msimamo wa kijamii na kisiasa wa Wakristo katika nchi za Mashariki,  Papa anafafanua Kardinali wa Iraq katika mazungumzo yake na Fides, haji kutetea na kulinda Wakristo. Papa sio mkuu wa jeshi. Kwa uhakika, Papa Francisko atawatia moyo Wakristo, atawaletea faraja na matumaini ya kuwasaidia kuvumilia, kuwa na matumaini na pia kushirikiana na raia wengine. Papa hawezi kufanya chochote isipokuwa hii ni kuwaleta na kuwaunganisha pamoja madhehbu yote. Anakuja kwa Wairaq wote, sio Wakristo tu. Anajua kwamba kila mtu ameteseka, sio Wakristo tu. Na kama Mchungaji, atahimiza Wakristo kukaa kwa imani, kutumaini, kujenga imani tena na wengine”.

Udugu wa kibinadamuna udugu wa kiroho:Watu wote walisteseka, wakristo, washia na Yazid

Patriaki wala hakubaliani hata na kanuni za uongo za wale wanaorudia kusema kwamba Papa anasafiri kwenda Iraq kukomesha mauaji ya kimbari ya Wakristo: “Ikiwa kulikuwa na mauaji ya kimbari, Patriaki Sako amekumbukusha, hiyo imeathiri kila mtu: Wakristo na zaidi wale Yazidi, lakini pia Waashia na Sunni, kwa idadi kubwa zaidi. Hatupaswi kuwatenganisha Wakristo na wengine, mateso ya Wakristo na yale ya wengine, kwa sababu kwa njia hiyo fikira za kimadhehebu zinakuwa siyo za kweli.  Kwa upande mwingine, Papa atazungumza juu ya udugu wa kibinadamu, na pia juu ya undugu wa kiroho. Kwa mfano, huko Uru, katika mkutano wa kidini, atarudia kwamba sisi ni ndugu kwa sababu imani katika Mungu mmoja hutufanya tuwe ndugu. Na atasema vya kutosha kuhusiana na vita itikadi, na  ugaidi. Wale ambao huleta usemi 'mauaji ya kimbari' mara nyingi hufanya hivyo kutekeleza malengo mengine, nia za kisiasa”.

Wafiadini ni zawadi yetu kwa Kanisa lote la Kristo

Katika ziara yake nchini Iraq, Mfuasi wa Petro, Mtume aliyeuawa shahidi juu ya Kilima cha Vatican, pia atakumbatia tukio la  wafia dini Wakristo wengi ambao wamejumuisha njia ya jumuiya hizo za kikanisa huko Baghdad na Mosul. Patriaki Mkuu wa Kikaldayo anashuhudia kile ambacho kilitokea katika mateso ya wafiadini wapya. Kufia dini Kardinali anakumbusha  sio ushujaa wa kujiua.  Kufia dini ni kielelezo cha imani na onesho  kuu la upendo. Sisi wa Makanisa ya Mashariki, katika nchi za ile iliyokuwa Mesopotamia ya zamani, hatujawahi kufurahiya uzuri wa ulimwengu. Kanisa hapa halijawahi kuwa Kanisa la kifalme, au Kanisa la Serikali. Kwa maana hiyo utukufu na uzuri wa Kanisa hili ni mambo ya undani inayojikita  katika maisha ya imani ya Wakristo. Na hawa wafia dini, sio wale wa zamani tu, bali pia wale wa leo, walitoa maisha yao kwa upendo wa Kristo. Wao ni utukufu wetu, na uzuri wetu. Ni zawadi yetu kwa Kanisa lote la Kristo”.

Kuwa na uvumilivu kama Mababu walivyobaki kwa uvumilivu 

Patriaki Sako pia anaonya dhidi ya hotuba za wale wanaosema kwamba Wakristo hawawezi kubaki nchi za Mashariki bila kupata msaada kutoka nje, na kwamba msaada wa nje ndio jambo muhimu katika kuzuia kutoweka kwa jumuiya za Kikristo asilia katika nchi za Mashariki. Hiyo amerudia Patriaki kuwa ni makosa sana. Tunaweza kubaki hapa kama mababa zetu walibaki, ambao waliweza kukabiliwa na shida kubwa kuliko zetu. Sisi sasa tunaweza kuondoka  lakini wao hawakuweza. Katika siku zao hakukuwa na magari na ndege. Walikuwa na uvumilivu, na tumaini kubwa kwa Mungu”. Hata hivyo hakuna mtu anayeweza kulazimisha kwa Wakristo wa Mashariki kubaki katika ardhi zao bila mapenzi yao. Lakini Wakristo wanabaki anajua Patriaki na kwamba  ikiwa wataona kuwa ni vizuri kuendelea kuishi maisha yao na Yesu mahali ambapo walizaliwa.  Kardinali Sako ameongeza “ Maisha hapa yamejaa shida na mambo machungu, lakini hata hapa unaweza kupata Heri, na kugundua hapa kwamba Injili sio mazungumzo. Katika hili, ukweli wa Kanisa una majukumu,  na kumekuwa na mapungufu katika kutekeleza kazi ya kitume kati ya watu. Na kuwasaidia kila mtu kufurahiya hazina ya imani.

04 March 2021, 10:46