Chanjo dhidi ya Covid-19 nchini Sudan Kusini Chanjo dhidi ya Covid-19 nchini Sudan Kusini 

Afrika Kusini:Wiki tano za tafakari ya kukuza tumaini jimboni Aliwal

Wiki tano za tafakari kwa ajili ya kukuza tumaini kwa waamini na kuwasadia kishinda hofu na woga uliotokana na janga la Covid-19,ndiyo mapango uliozinduliwa katika jimbo la Aliwal,nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha Kwaresima 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika kipindi cha Kwaresima mwaka 2021 jimbo katoliki  la Aliwal nchini Afrika Kusini, wameandaa tafakari kwa wiki tano, lenye kuongozwa na  kauli mbiu: “Jumuiya ndogo ndogo za Kristo: vidokezo vya tafakari”. Wazo hilo linaona uchaguzi wa mada moja kwa kila wiki ambayo waamini wanaalikwa kutafakari. Atakaye wasindikiza katika tafakari hizo atakuwa ni kiongozi mkuu wa jimbo hilo, Askofu Joseph Kizito, ambaye amejiwekea lengo la kujenga imani kwa waamini, ambao bado wanaogopeshwa na dharura ya kiafya. Akizungumza kuhusu suala hilo Askofu Kizito amesema bado kuna hisia ya kujitenga na hofu kati ya watu. Katika mpango huu, wanataka kurudisha kuunda hali ya akili iliyokuwa ya Kanisa kabla ya virusi vya corona kuanza. Wiki ya kwanza ya tafakari kuhusu woga, ili kusaidia watu kuelewa kwamba inawezekana kuhudhuria kanisani kwa ajili ya maombi binafsi, kila wakati kwa kuheshimu kanuni zote za kupambana na maambukizo yanayoendelea.

Wiki ya pili, tafakari itajikita juu ya  ukosefu wa ajira, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linazungukiajanga hili, na umaskini uliosababishwa nalo na ambao umeathiri sehemu kubwa ya idadi ya watu. Wafanyabiashara wamefunga vilago na milango yao na watu wengi wamepoteza kazi na kuishia katika unyong’onyevu mkubwa kwa mujibu wa maelezo ya Askofu Kizito. Katika hili, watachagua maandishi kutoka Maandiko Matakatifu ambayo yanazungumza tumaini kama vile simulizi la kibiblia kuhusu Ibrahimu alivyo ambiwa aache kila kitu ili aenda mahali hasikokujua.

Mada ya tatu, itakuwa juu ya kifo: hasa, katika juma la tatu, ambalo Wakatoliki wataalikwa kuombea roho za wapendwa wao waliopoteza maisha yo kwa sababu ya janga la viruso vya Corona, zaidi wale ambao hawakuweza kusindikiza hatua ya mwisho kwa sababu ya maambukizo zilizuiwa ibada za mazishi.  Kwa mujibu wa Askofu amesema kuwa moha ya Parokia za jimbo lake liliona watu 15 wakifariki kwa miezi miwili tu bila kupata mazishi yanayostahili.

tafakari ya matumaini itakuwa katika mada  msingi ya Juma la Nne, wakati Juma la mwisho wakatoliki wa jimbo la Aliwal watashauriwa kusali kwa ajili ya uongofu wa mioyo ya wahalifu katika Nchi. Hii ni kutokana na kwamba wakati wa Karantini, Parokia nyingi zimekumbwa na wizi na uharibifu wa mali amebainisha Askofu: “Katika jimbo langu uhalifu umeathiri takriban makanisa 55 ambayo zimevamiwa na majambazi na wahalifu kwa kuiba vifaa vitakatifu vya misa lakini pia vifaa vya kiteknolojia kama kompyuta, maikrofoni na spika. Hatima hiyo hiyo ilikumbwa na nyumba nyingi za kidini pia nyumba za watawa”. Kwa njia hiyo ni matumaini ya Askofu Kizito kuwa mpango wa sala na tafakari inaweza kusaidia kumaliza mambo haya ya wizi na uharibifu.

21 February 2021, 11:26