Katika katekesi kuhusu familia,Tawadros anasisitizia juu ya kuwakomboa watoto na vijana dhidi mambo ya uongo wa ulimwengu Katika katekesi kuhusu familia,Tawadros anasisitizia juu ya kuwakomboa watoto na vijana dhidi mambo ya uongo wa ulimwengu 

Misri,Tawadros:tuwakomboe watoto dhidi ya mahitaji ya uongo!

Kutokana na kutoweza kufungua milango ya Kanisa kuu kwa ajili ya mikutano ya watu wengi,katekesi za Patriaki zinatangazwa kupitia njia ya vyombo vya habari vya Upatriaki na Patriaki Tawadros ameamua kuzindua mfululizo wa mada zinazohusu masuala ya sasa na mahitaji yanayohusiana na maisha ya familia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Covid-19 imeleta ugumu wa kutoweza kushiriki kikamilifu katika uwepo wa mikusanyiko iliyojaa na ambayo imesababisha familia nyingi kutumia wakati mwingi kuwa pamoja katika nyumba zao zilizofungwa. Hali hii imempa msukumo Patriaki wa kiorthodox wa Kikoptiki Tawadros II kukabaliana na hali ya sasa pia utamaduni wa katekesi ya kila wiki ambayo alikuwa akifanya kila Jumatano jioni katika Kanisa kuu la Kikoptiki jijini Cairo. Kwa wiki kadhaa, kwa kuwa haikuwezekana kufungua milango ya Kanisa kuu kwa ajili ya mikutano ya watu wengi, katekesi za Patraiki zinatangazwa kupitia njia ya vyombo vya habari vya Upatriaki na Patriaki ameamua kuzindua mfululizo wa mada zinazohusu masuala ya sasa na mahitaji yanayohusiana na maisha ya familia ili familia ziweze kufuatilia mikutano hata wakiwa nyumbani, kupata faida na faraja.

Katika katekesi iliyotangazwa siku ya Jumatano tarehe 17 Februari 2021, Patriaki Tawadros II  amesisitizia maoni na vigezo vya kuthaminiwa katika elimu ya watoto. Hasa, Patriaki ameshauri kufanya kila linalowezekana kuwakomboa watoto kutokana na kuzingirwa na mahitaji ya uwongo ambayo wamepewa kupitia utandawazi wa sasa wa watumiaji.  Watoto wa kike na kiume  amependekeza Patriaki kuwa lazima wasaidiwe kuondoa vitu ambavyo havihitajiki, kupunguza matumizi ya vitu visivyo na maana, ili kuweza kufurahia zawadi za  kazi ya uumbaji na  upendo wa kifamilia, kutambua thamani ya wakati na kazi ya subira, kwa kuwasaidia  kujiondoa kwenye ghasia na udikteta wa kutka kila kitu mara moja tabia  ambayo hutumia  kama zana hata ya  mawasiliano  ya haraka iliyohakikishiwa na teknolojia mpya za digitali. Tawadros pia amewaaalika  kueneza kwa  mifano kwa watoto wa kike kuheshimu mazingira na utulivu katika utumiaji wa maliasili, wakianza na maji.

Tayari mnamo Julai 2015, Patriaki Tawadros II, wakati wa ziara yake ya kichungaji huko Alexandria Misri, alikuwa ametaka kuhudhuria mkutano wa tafakari na sala na zaidi ya wanawake ishirini wa makuhani wa Kikoptiki- Kiorthodox wanaofanya kazi katika sekta ya mashariki ya jiji kuu la Misri. Katika tukio hilo, Patriaki alifanya tafakari yake kwa kuchanganya maoni juu ya maisha na wito wa kuhani na tafakari juu ya ukweli wa uzazi na ndoa kama ilivyoainishwa katika maandiko ya kibiblia. Katika Makanisa ya Kikoptiki kuna uwezekano wa kuchagua kuendelea na ukuhani  wa wale ambao wanaishi useja na kati ya wale ambao wameoa, wakati Maaskofu wote wanatoka katika mamonasteri ya  watawa na hawahoi.

Mnamo Februari 2016, wakati wa mkutano wa katekesi uliofanyika katika kitongoji cha Guizeh,huko Cairo, Patriaki Tawadros alisisitia juu unyanyasaji wa nyumbani, ambao wanawake na watoto ni waathiriwa, akielezea jambo hili kama janga kubwa la kijamii, ambalo lina athari kubwa kwa maisha ya watu na pia kwa kuishi pamoja. Katika fursa hiyo, akinukuu maneno ya Yesu katika Mahubiri ya Mlimani (Heri wapole, kwa sababu watairithi dunia), Patriaki Tawadros alisisitiza kwamba hata shida za ndoa na familia lazima zitatuliwe kwa upole, kufuatia mafundisho ya kiinjili ya upole, na ndiyo iwe tabia muhimu ya njia ya maisha ya wale wanaomfuata Yesu.

20 February 2021, 12:43