Tafuta

SHAMBULIZI NCHINI DRC LIMESABABISHA KIFO CHA MWANADIPLOMASIA,AFISA WAKE NA DREVA WA SHIRIKA LA MPANGO NA CHAKULA (WFP) SHAMBULIZI NCHINI DRC LIMESABABISHA KIFO CHA MWANADIPLOMASIA,AFISA WAKE NA DREVA WA SHIRIKA LA MPANGO NA CHAKULA (WFP) 

Baraza la kiekumene la Makanisa kulaani shambulio la utume wa UN!

Baraza la kiekuemene la Makanisa linalaani vikali shambulio la utume wa Umoja wa Mataifa ambapo umepoteza maisha ya watu watatu.Balozi wa Italia,afisa wake na Dreva wa Shirika la Mpango na Chakula (WFP)

Na Angela Rwezaula – Vatican.

Katibu Mkuu wa Mpito wa Baraza la kiekumene la Makanisa (Coe), Mchungaji Ioan Sauca, amelaani shambulio la msafara wa Umoja wa Mataifa (UN) uliotokea tarehe 22 Februari 2021 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mashariki ambapo balozi wa Italia Bwana Luca Attanasio, afisa wake Vittorio Iacovacci,na dereva, Mustapha Milambo, waliuawa. Mchungaji anasema kuwa "Mwanadiplomasia huyo alikuwa kwenye safari ya amani kwenda Rutshuru akiwa ndani ya magari ya  Shirika la Mpango wa Chakula wa la Umoja wa wa Mataifa (WFP)".

“Tunatoa wito wa kukomeshwa kwa mashambulizi haya yasiyo na maana ambayo yanakiuka ulinzi muhimu wa wafanyakazi wa kibinadamu", amesema Mchungaji Sauca.  Kwa kuongezea amesema "Tunatoa sala zetu kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao na tunawapa pole nyingi”.  Katika taarifa yake, Baraza la kiekumena la  Makanisa linabainisha kuwa uvamizi wa ujumbe wa UN umeundwa katika msingi mpana wa mateso yanayosababishwa na ukatili wa vikundi vyenye silaha katika mkoa wa kaskazini-mashariki na kuongeza kusema kuwa, "hii yote inaoneshwa na historia ndefu na ngumu ya ukatili wa ukabila mpakani, kutokana na kuingiliwa kutoka nje na kutokana na unyonyaji wa rasilimali nyingi za madini, migogoro inayotokea huko ina athari katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa".

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa mpito  wa Coe, anasema "kile kilichotokea huko kinapaswa kusimamisha kwa njia ya jitihada za jumuiya ya kimataifa kwa ajili ya amani, usalama na haki katika eneo hilo". Wajibu wao wote  wa kimaadili ni kusaidia jamii za wenyeji ambazo zimejaribiwa kwa miongo kadhaa na mateso mabaya amesisitiza Mchungaji Sauca.

24 February 2021, 16:03