TAPOLOGO ni mpango kwa ajili ya wagonjwa wa HIV-AIDS nchini  Afrika Kusini ulioanzishwa na Askofu wa Dowling TAPOLOGO ni mpango kwa ajili ya wagonjwa wa HIV-AIDS nchini Afrika Kusini ulioanzishwa na Askofu wa Dowling 

Afrika:Wajesuit watoa wito,Corona haipaswi kusahau janga la VVU

Katika barua iliyochapishwa kwa mtazamo wa Mkutano wa Ajan (Africa Jesuit Aids Network)uliopangwa kuanzia tarehe 4-6 Februari,rais wa Jcam amesema mabadiliko ya umakini wa ulimwengu katika Virusi vya corona umesababisha kupungua kwa rasilimali za vita dhidi ya UKIMWI,kana kwamba ugonjwa huo tayari ulikuwa umeshindwa.Lakini ni mtazamo potofu kwa sababu VVU ni tishio.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Janga la Covid-19 halipaswi kutufanya tusahau kwamba virusi vya UKIMWI  bado ni tishio kubwa kwa Afrika na Madagascar. Haya yamesema na Baraza la  Wajesuit kwa ajili ya  Bara (Jcam), ukihimiza uwepo wa mantendo ya nguvu na kuratibu ili kukabiliana na hali hii kubwa. Katika barua iliyochapishwa kwa mtazamo wa Mkutano wa Ajan  (Africa Jesuit Aids Network) yaani Mtandao wa usaidizi wa Wajesuit barani Afrika, uliopangwa kufanyika  kuanzia tarehe 4 hadi 6 Februari 2021, rais wa Jcam, Padre Agbonkhianmeghe Orobator amebainisha kwamba mabadiliko ya umakini wa ulimwengu katika Virusi vya corona umesababisha kupungua kwa rasilimali ya mapambano dhidi ya UKIMWI, kana kwamba ugonjwa huu tayari ulikuwa umeshindwa. Lakini kumbe huu ni mtazamo potofu kwa sababu virusi vya Ukimwi (VVU) ni tishio na kuendelea kuwa tishio.

Sio hivyo tu, Covid-19 imekuwa na athari nzito kwa watu wanaougua UKIMWI kwa sababu mbili. Kwa mujibu wa Padri Orobator anaelezea kuwa “kwanza, wako katika hatari zaidi ya ugonjwa wa corona kutokana na kinga ya mwili ambayo tayari imedhoofishwa na VVU”; pili, wagonjwa hawa sasa “hawana tena rasilimali sawa na hapo awali kujaribu kushinda ugonjwa wao”. Kwa njia hiyo, pendekezo la mtawa huyo ni “kutofautisha vyanzo vya fedha ,kwa namna ya kutoweza kutegemea wafadhili wa nje tu, na kuweza kujibu kweli mahitaji ya waamini kulingana na ishara za nyakati” .

Ulimwengu, kiukweli, anahitimisha mkurugenzi wa Jcam, kwamba unaonesha  zaidi na zaidi kuongezeka kwa matokeo ya ugonjwa, ukosefu wa usawa, ukiambatana na ukosefu wa upatikanaji wa dawa na dawa kwa masikini. Kwa maana hii, Wajesuit wanathibitisha kujitoa kwao katika utetezi kwa niaba ya afya ya umma na haki kijamii. Kwa upande wake, mkurugenzi wa Ajan, Padre Ismael Matambura, amesema kuwa waanalenga kuboresha uwezo wa mwili, kutathmini, kufuatilia na kupima kuhusiana na athari za UKIMWI katika eneo hilo. Kwa hili, mtandao utawekeza katika mafunzo na kuzindua mipango maalum, ukiangalia Malengo ya maendeleo endelevu na vipaumbele vya afya ya umma ulimwenguni.

Ajan ikiwa na makao makuu katika Jimbo kuu la Nairobi, Kenya, inaratibu jitihada na Wajumbe wa Shirika la Kijesuit katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI barani Afrika kupitia mitandao, mawasiliano, kujenga uwezo, utetezi, kutafuta fedha na uhamasishaji wa rasilimali. Kwa undani zaidi kiungo hiki  hutoa huduma kama vile utunzaji  na matibabu ya VVU, kutoa ushauri wa kiroho na kisaikolojia, pia maendeleo muhimu ya watu kwa wagonjwa kupitia msaada wa maisha na msaada wa elimu kwa yatima na watoto walio katika mazingira magumu.

03 February 2021, 13:11