Umakini unahitajika barani Afrika kufuatia na mlipuko wa pili wa Covid-19 Umakini unahitajika barani Afrika kufuatia na mlipuko wa pili wa Covid-19 

Afrika:Afrika inabaki kati ya mabara yaliyoathiriwa kidogo &kaa chonjo na wimbi la pili!

Afrika inabaki kati ya mabara ambayo hayakuadhiriwa sana na Covid-19 lakini Kanisa linahimiza kuwa na tahadhari zaidi hasa katika wimbi la pili la covid-19 ambalo linazidi kuona mtu mmoja mmoja katika jamii anaondoka kwa sababu ya mfumo wa hewa.Viongozi wa Kanisa wanaomba watu wote warudie njia za kuthibiti ambazo walikuwa nazo mwaka jana.

Na Sr. Angela Rweaula - Vatican

Kuna vipimo vichache, hatua zake zilizo huru na wakati virusi vipya vinavyojificha  vinahashiria kuhatarisha kazi iliyofanywa hadi sasa. Mataifa kadhaa ya Afrika sasa yanapata wimbi la pili la janga la covid-19, pia kwa sababu ya kuenea katika miji mikubwa  hasa Afrika Kusini. Taarifa hiyo inakuja moja kwa moja kutoka kwa wawakilishi wa dini, kama Padre Charles Chilufya, mratibu wa Kikosi Kazi cha Afrika cha Tume ya Vatican Covid-19 na mkurugenzi wa Ofisi ya Sheria na Ekolojia ya Baraza la  Wajesuit wa Afrika na Madagascar, ambaye anabainisha kuwa nchi kadhaa ziliripoti ongezeko jipya la kesi kwa mwezi uliopita.

Wasiwasi  huo ullishirikishwa hata Baraza la Maaskofu katoliki nchini Tanzania ambao, katika ujumbe wao mrefu tarehe 26  Januari 2021  umewaonya waamini juu ya wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya Corona  ambayo imesababisha kuongezeka kwa vifo.  “Tanzania sio kisiwa. Lazima tujitetee, kuchukua tahadhari na kumwomba Mungu kwa nguvu zetu zote ili janga hili lisitufikie”, Askofu mkuu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Tanzania (TEC) alisema. Kwa njia hiyo Maaskofu wanawaomba  raia wote wazidishe kujitoa katika vita dhidi ya virusi  kwa kutumia silaha zote za kiroho, za mwili, za kisayansi na za kijamii. “Hatuachi kuwaomba, kuweka umbali wa kijamii, kunawa na kusafisha mikono, kuvaa barakoa, na kuchukua hatua zinazohitajika tunapoona dalili za ugonjwa na kuzuia mikusanyiko ambayo inaweza kuwa hatari”.

Nchini Zambia, Jimbo katoliki la Ndola linafikiria kusitisha sherehe za kiliturujia kwa sababu  wanasema “katika parokia zetu nyingi na taasisi zetu, hatua za kinga za COVID-19 zimelegezwa sana na, wakati mwingine, hata zimeachwa kabisa”. Katika taarifa ya tarehe 26 Januari ilionya juu ya parokia tisa zilizofungwa kwa sababu ya idadi kubwa ya kesi chanya zilizopatikana. Wakati huo huo nchini Nigeria inajiandaa kupokea dozi zake za kwanza za chanjo, wakuu wa Kanisa la Ibadan wamejaribu kupunguza hofu ya watu juu ya kuaminika kwake. Ili kufanya hivyo, wameomba kwamba madaktari waruhusiwe kutoa chanjo za covid-19 zinazoingia Nigeria kwa vipimo stahiki ili kujenga imani kati ya watu, ili wapate matibabu kwa hiari.

Kufikia sasa, Afrika imeathiriwa kidogo zaidi kati ya mabara, kwani kwa mujibu wa data za hivi karibuni zilizotolewa na Wizara ya Afya ya Italia, visa 2,523,516 vimethibitishwa, vifo 60,577. Ni eneo la Pasifiki ya magharibi tu ambalo limekuwa na chini. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni  (WHO) wanathibitisha kuwa hii inatokana kwamba ni sehemu ambayo ina idadi ya watu wenye uwiano wa umri mdogo na ni watu wahamiaji.

05 February 2021, 14:14