Tafuta

Wakati wa maadhimisho ya Misa ya mkesha wa Noeli na Patriaki Kirill wa Moscow, Urusi. Wakati wa maadhimisho ya Misa ya mkesha wa Noeli na Patriaki Kirill wa Moscow, Urusi. 

Patriaki wa Moscow:amini Mungu ili kushinda majaribu!

Katika fursa ya Noeli ya Kiorthodox, Patriaki wa Moscow ametoa ujumbe wake akihimiza kumwamini Mungu ili kushinda majaribu.Amebainisha hayo wakati wa Misa ya Mkesha wa Noeli katika Kanisa Kuu la Kiorthodox la Kristo Mfalme,kufuatana na kalenda ya kijuliani kati ya tarehe 6 na 7 Januari 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Nilipowageukia ninyi nyote hapa au kuwepo mahali hapa, wakati wa Pasaka, kwa dhati hapakuwapo na yoyote katika Kanisa kuu la Kristo Mfalme. Lakini sasa ninasikia sauti kwa maana ya uwepo wa watu katika hekalu. Na ikiwa tunazungumza kile ambacho kinaendelea kutokea leo hii kwetu sisi ina maana kuwa virusi vya corona ambavyo kweli vimekuwa ni jaribu kubwa kwa watu wetu na linaendelea kwa taratibu kutoweka. Ni maneno ya tumaini yaliyotamkwa na Patriaki Kirill wa Moscow, kabla ya kuanza liturujia ya Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwan,a sherehe za Kanisa la Kiorthodox ambazo zinafuata kalenda ya kijuliani na ya Makanisa Katoliki ya Mashariki, mara baada ya shere za Noeli kwa Kanisa Katoliki na katika muktadha huu, misa hiyo ilifanyika kati ya usiku wa tarehe 6 na 7 Januari 2021.

Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox nchini Urusi katika ujumbe wake wa Noeli ambao ulisikika moja kwa moja katika majukwaa mawili,  Luninga ya kitaifa na Jukwaa la Upatriaki, amebainisha jinsi ilivyo siku kuu ya wokovu wa dunia ,mahali ambapo inaalika kutafakari kwa kina maana yake ya kiroho ya kudumu na wakati huo huo kuwa ni ufunguo kwa ubinadamu wote. Hasa katika nyakati hizi ngumu mahali mbapo kuna uhitaji maombi yasiyo isha kwa Mungu ambaye atamwezesha mtu kupona na kurudia katika uzuri wake asili, amesema.

Watu wa mataifa ameendelea kusema Patriaki Kirill, wanaishi katika majaribu magumu ya ugojnwa mpya, na mioyo ya watu yenye kuwa na hofu, mhemuka wa wakati ujai, na kwa namna ya pekee lazima kujtoa bidiii ya sala ya pamoja na binafsi, ili kumwomba Bwana msaada muhimu kwa wale wote walioambukizwa na ambao hawajuhi matokeo yake. Kutokana na hili ndipo ametoa ushauri wa kuinua sala kwa Mwenyezi Mungu ili apyaishe ndani mwao nguvu ya kiakili na mwili, kuwahakikishia wagonjwa uponywaji wa haraka na msaada kwa madaktari na wahudumu wote wa kiafya ili kupambana bila kuchoka kwa ajili ya afya na maisha yao.

Mungu kama mlinizi na wa kuongoza maisha ya safari yetu ya mahangaiko hivyo ni kumwomba bila woga kwa ajili ya maisha yetu. Wakumbuke kuwa hakuna shida ambayo inaweza kumwondoa undani wa kuhifadhi imani hai na ambayo ni kumwamini Mungu kwa kila kitu. Na zaidi, pigo la majaribu yaliyo mkubwa mwanadamu lazima yapokelewe bila kulalamika kwa sababu ikiwa wanaamini Yeye, amesema watatakatifuzwa, kwa kuwa Mungu yupo pamoja nao, kama Kanisa la Kristo linavyoimba wakati wa  siku kuu ya Noeli. Ni lazima kuunganisha maombi yao  kwa namna kwamba mwanga wa Mungu uangaze taabu za maisha, ili mioyo yao iliyopendeka na nyenyekevu kama mtoto wa Bethlehemu, ipokeee kwa heshima ya Mwokozi aliyekuja ulimwenguni.

Ni kwa njia hiyo tu, katika siku takatifu za maadhimisho ya Noeli yatapata maana ya furaha na utajiri wa matumainini chini ya vazi la huruma la Bwana mtukufu na kwa kila huduma inayotolewa kwa jina lake katika kutunza kwa  upendo wa kikristo jirani anayeteseka amesisitiza Patriaki Kirill. Kwa kuhitimisha mkuu wa Kanisa la Kiorthodox huko Urusi anasema, Mungu aweze kuangaza watu wa nchi kwa Mwanga wake wa fahamu, awabariki na amani na kuwasaidia wote kutumiza wajibu wao wa pamoja ili wakati uliopo na ujao wa sayari hii. Mtoto Yesu aweze kuzindua upendo na maelewano katika familia zao, aweze kuwalinda vijana na watu wote wadhambi na makosa hatari.

08 January 2021, 11:32