Tafuta

2020.01.16 Mandamano kwa ajili ya amani huko Kalcuta wakati wa Wiki ya maombi kwa ajili ya Umoja wa Mataifa 2020.01.16 Mandamano kwa ajili ya amani huko Kalcuta wakati wa Wiki ya maombi kwa ajili ya Umoja wa Mataifa  

Wiki ya Maombi kwa ajili ya umoja wa Kikristo:Wcc yazindua biblia ya kiarabu mtandaoni

Katika fursa ya Wiki ya Maombi kwa ajili ya umoja wa Kikristo kuanzia tarehe 18 hadi 25 ya mwezi Januari kila mwaka,Baraza la Makanisa ulimwenguni, mwaka huu wamezindua Biblia katika lugha ya kiarabu kwenye kwenye mtandao itakayoruhusu wakristo wa uarabuni kishiriki sala na tafakari wakiwa nyumbani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa mara ya kwanza, Wakristo wanaozungumza Kiarabu wanaweza pia kushiriki mwaka huu katika maombi na tafakari za Kibiblia ya Wiki ya Umoja kuombea umoja wa kikristo katika lugha yao ya nyumbani shukrani kwa tafsiri ya  Kiarabu ya programu mpya ya kibiblia iliyozinduliwa mnamo 2016 na Baraza la Makanisa Ulimwenguni(Wcc). Programu iliyoko sasa kwenye (App) ilitengenezwa na ‘YouVersion’ na tafsiri hiyo ilishughulikiwa na Baraza la Makanisa ya Mashariki ya (Mecc).

Hii ni habari mpya ambayo ni muhimu sana mwaka huu ambapo katika sehemu nyingi za za tukio la Wiki ya Kiekumene zinafanyika kwa njia ya mtandao. Amebainisha hayo mkurugenzi wa mawasiliano wa Baraza la Makanisa ya Mashariki (Mecc). Bi Huguette Salameh: “Katika Mashariki, sherehe za kiutamaduni za Wiki ya Maombi zimesitishwa kwa sababu ya janga, kwa njia hiyo tunafurahi hasa kuweza kuwapa Wakristo katika eneo hili zana mpya ya kuweza kushiriki wakiwa nyumbani kupitia kompyuta zao au vifaa vya simu zao za mikononi” amethibitisha.

Nyenzo mpya kwa Kiarabu, ameelezea Marianne Ejdersten, mkurugenzi wa mawasiliano ya Baraza la Makanisa uimwengini (WCC) kuwa imeongezwa kwenye matoleo ya 2,062 ya Biblia katika lugha 1,372, zilizotolewa na programu ambayo hadi sasa imewekwa kwenye vifaa vya kudumu au app milioni zaidi ya 450  ulimwenguni kote, kuruhusu watumiaji kusoma Biblia, kushirikisha aya kupitia mitandao  ya kijamii na kuweka hata alama vifungu wanavyopenda. Ni muhimu kuweza kuomba kwa lugha yao wenyewe, na lugha ya moyo wao”, amesisitiza Ejdersten.

Tangu 2016, tafakari na maombi ya kibiblia ya Wiki ya Maombi ya Umoja wa Kikristo imekuwa ikipatikana kwenye programu ya ‘YouVersion Bible’ kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kihispania na Kireno. Wiki ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo huadhimishwa, kila mwaka, kuanzia tarehe 18 hadi 25 Januari. Tume ya Kimataifa iliyoundwa na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha  Umoja wa Kikristo (PCPUC) na Tume ya Imani na Katiba ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni imekabidhi uchaguzi wa mada na uandishi wa msaada wa masomo na kwa maombi kwa jumuiya  ya watawa marekebisho wa huko Grandchamp, Uswizi. Mada iliyochaguliwa imeongozwa na Injili ya Yohana na inafupishwa kwa maneno yasemayo “Kaeni katika pendo langu: mtazaa matunda mengi” (Yn 15: 5-9).

20 January 2021, 14:12