Tafuta

INDONESIA EARTHQUAKE INDONESIA EARTHQUAKE 

Indonesia:CEI imetoa euro 500elfu kwa watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi

Baraza la maaskofu nchini Italia limetangaza kutoa msaada wa Euro 500elfu kwa ajili ya watu wa Indonesia waliopatwa na tememeko la ardhi hasa katika eneo la Sulawezi.Naye Mkurugenzi wa Caritas nchini Indonesia Padre Fredy Rante Taruk,amethibitisha kuwa maparokia mahalia ya Mamuju na Poliwali imebidi wachukue uamuzi wa haraka wa kufungua Kituo cha dharura kwa ajili ya kuwapokea watu wengi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika harakati za kutoa msaada kwa watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi kisiwani Silowesi nchini Indonesia, kati ya usiku wa manane Alhamisi na Ijumaa ya wiki hii,  Baraza la Maaskofu nchini Italia wametoa salam zao za rambi rambi na ukaribu wa watu huku wakiwakikishia sala zao marehemu na  waathiriwa wote, familia na majeruhi. Na zaidi Baraza limetangaza kutoa msaada wa dhati wa Euro 500elfu kwa ajili ya watu hao.

Hata hivyo Caritas ya Indonesida kwa sasa inaendelea na harakati za kutoa msaada ambao tayari kwa msaada wa Caritas ya Italia ilikuwa imekwisha tuma tangu Ijumaa tarehe 15 Januari 2021, ambao ni mchango mkubwa  kwa ajili ya kuwasaidia  watu kama ilivyoelezwa hata katika tovuti ya Caritas ya Italia: www.caritas.it.

Naye  Mkurugenzi wa Caritas nchini Indonesaia Padre Fredy Rante Taruk, amethibitisha kuwa maparokia mahalia ya Mamuju na Poliwali imebidi wachukue uamuzi wa haraka wa kufungua Kituo cha dharura kwa ajili ya kuwapokea watu wengi kwa sasa ambao hawana mahali pa kukaa, wakati idadi kubwa ya watu wa kujitolea wakindelea kwenda maeneo yaliyokumbwa sana ili kupata taarifa zaidi wakiwasaidia na kukusanya takwimu za kile ambacho kinahitajika zaidi.

16 January 2021, 19:20