Kardinali Berhaneyesus Souraphiel,Askofu Mkuu wa Ethiopia amewashauri watu wote kulinda maisha ya binadamu na kuheshimu katiba ya nchi kwa ajili ya wema wa wote Kardinali Berhaneyesus Souraphiel,Askofu Mkuu wa Ethiopia amewashauri watu wote kulinda maisha ya binadamu na kuheshimu katiba ya nchi kwa ajili ya wema wa wote 

Ethiopia,Kard.Souraphiel:Lindeni maisha ya binadamu&kuheshimu katiba

Katika ujumbe wake Kardinali Souraphiel,Askofu Mkuu wa Ethiopia kwa ajili ya Siku kuu ya Noeli ambayo imeadhimishwa tarehe 7 Januari 2021 kulingana na kalendea ya kijuliani amehimiza kulinda maisha ya binadamu na kuheshimi katiba hasa katika muktadha wa hali halisi ya mgogoro uliopo ndani ya nchi hiyo wa Mkoa wa Tigray,ambamo wamekufa watu wengi na kusababisha maelfu ya wakimbizi wa ndani.

Na Sr Angela Rwezaula - Vatican

Kulinda maisha ya binadamu na kuheshimu katiba ndiyo mambo muhimu ya ujumbe wa Kardinali Berhaneyesus Souraphiel, Askofu Mkuu wa Ethiopia wakati wa misa ya Siku kuu ya Noeli ambayo imeadhimishwa tarehe 7 Januari 2021 kulingana na kalenda ya kijuliani. Kilio kiishe na mateso ya wengi, unyonyaji na vifo vya watu wengi katika Mkoa wa Tigray vikome ambavyo karibu miezi miwili vinaendelea vilivyowekwa na Serikali ya dhidi ya mamlaka mahali mara baada ya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa kitaifa katika Mkoa. Kutokana na hili ndipo wito wa Kardinali Souraphiel kwa sehemu zote mbili ili waongeze nguvu za kuhakikisha usalama na amani nchini Ethiopia pamoja na Serikali ya hakika na kulinda haki za binadamu.

Na kwa upande wa watu wote wa Ethiopia, wameshauliwa kuwa wahudumu wa amani: Tunapaswa kuishi pamoja kama kaka na dada, mbali na makabila yetu, koo, rangi, umri na jinsia na ili tuwa familia moja ambayo inatusaida na kusaidiana pamoja na kutunza umoja” ameandika Kardinali. Watu wa Mungu wanashikamana katika upendo na kuna haja ya mshikamano na wakimbizi waliorundikana ndani wakati huu wa siku kuu za Noeli. Kardinali amehimiza kuwasaidia kwa namna ya pekee: “Kwa upendo wa Bwana wetu, ninawatia moyo kufanya Noeli kwa kutumiza matendo ya upendo, kwa sababu Bwana anaendelea kutuomba kuwasaidia wenye kuhitaji. Sisi sote ni wadeni wa kilipa na deni hilo ni kuwa wema wa upendo mbele ya jirani”.

Hatimaye kwa kutazama muktadha wa Covid-19 ambayo imesababaisha vifo vya watu karibia elfu mbili na maambukizi mengi zaidi, kiongozi huyo amewaalika waamini wawe makini kujilinda na virus ambavyo vinawakilisha hatari kubwa ulimwengunu na katika Nchi yao. “Fuateni sheria za kuzuia maambukizi amehitimisha huku akiwasalimia watu wote wa Ethiopnia ambao wanaishi nchi za Nje, wagonjwa na wafungwa ili kwa namna moja au nyingine washerehekee kwa furaha ya Noeli.

08 January 2021, 12:04