Matumaini ya Askofu Mkuu Freddy Bretón Martínez,wa Santiago na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Dominika kuhusu mwaka  2021. Matumaini ya Askofu Mkuu Freddy Bretón Martínez,wa Santiago na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Dominika kuhusu mwaka 2021. 

DOMINIKA:vurugu dhidi ya wanawake na familia zinazidi!

Mada za unyanyasaji dhidi ya wanawake na familia zinaendelea kuchochea jeraha na kusababisha dhiki kwa mamia ya familia katika jamhuri ya Dominika kwa maana hiyo lazima kutafuta kupanda amani kwa 2021.Ndiyo wito wa maaskofu katoliki katika kisiwa hicho.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Askofu Mkuu Freddy Bretón Martínez, wa Santiago na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Dominika, anatarajia kuwa mwaka 2021 nchi inaweza kuwa na mfumo mzuri wa kitaifa na kuelezea matumaini yake katika mwaka mpya kwamba hata kiburi kinaweza kupungua katika ngazi zote na kwamba vijana wanaweza kupewa fursa zaidi za kazi na elimu. Katika barua yake aliyotuma kwenye Shirika la habari za kimisonari Fides, Askofu Mkuu Bretón Martínez pia anatumaini kwamba mwamko zaidi utakuwa kati ya raia na kwamba heshima inaweza kutawala, ili kusiwe na uchokozi tena, ubakaji na mauaji ya wanawake.

Maneno ya Askofu Mkuu wa Santiago yanakuwa mwangwi kwa yale yaliyotolewa pia na Askofu Jesús Castro Marte, wa jimbo la Nuestra Señora de La Altagracia”, Mama yetu wa Neema Kuu” katika siku ya Jumapili tarehe 3 Januari 2021 ambapo alilalamika kwa umma kwa kile ambacho kilitokea Kisiwani Carribien  wa maujai ya wanawake wawili ambavyo vimekuwa uchungu wa kuanza enzi mpya ya 2021 ya matukio mawili yaliyo  mabaya sana. Vifo hivyo vilivyotokea kwa masaa 48 kwa wanawake, vilisababisha uchungu usio na mfano. Alilaani na kuomba hali hii iishe.  Jamii yao imeinama kila siku katika vurugu. Je hadi lini hali hiyo itaisha katika umaskini wa kijamii? Aliuliza katika kuandikiwa kwenye mtandao wa kijamii “Twitter’. Askofu Castro Marte aliogeza kuseme “Mada za unyanyasaji dhidi ya wanawake na familia zinaendelea kuchochea jeraha na kusababisha dhiki kwa mamia ya familia katika Jamhuri ya Dominika, tunapaswa kutafuta kupanda amani kwa 2021”.

06 January 2021, 14:59