Patriaki Bartholomew I amepata chanjo ya dhidi ya  COVID-19 huko Instanbul Patriaki Bartholomew I amepata chanjo ya dhidi ya COVID-19 huko Instanbul 

Bartholomew I:Katika janga hili ni wito wa nguvu wa kuheshimu asili!

Patriaki wa Kiorthodox wa kiekumene alifungua toleo la nne la Mkutano wa Halki kuhusu uwajibikaji wa uendelevu wa mazingira.Kwa mujibu wape:mgogoro wa Covid siyo tendo la kulipiza kisasi kutoka kwa Mungu,lakini ni kutoa msukumo zaidi wa kuheshimu mazingira.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika ufunguzi wa Mkutano wa nne Halki, Patriaki wa Kiorthodox Bartholomew I amejikita kutoa wito kufanya  mabadiliko katika  mgogoro wa kiekolojia ili kuupatia nguvu uzuri ambao umechafuliwa na mahali ambamo unatokea. Kwa ushiriki wa wataalam wengi katika mkutano huo,  Patriaki huyo  amejikita katika tafakari kuhusu janga la sasa  la covid-19, katika uhusiano na mazingira na athari zake juu maisha ya sayari. Wakuu wa Mkutano huo wa Halki wanakumbusha jinis ambavyo wamekuwa daima wakiongozwa na thamani za mazungumzo na ushirikiano, na ndizo zinahitajika kwa kipindi  hiki kilicho shambuliwa na virusi ulimwenguni. Patriaki amesisitiza kwamba, wanaamini kuwa kila tumaini la kweli la uongofu katika masuala ya hali ya hewa  yanahitaji kwanza mabadiliko ya kina kwa namna ambayo kuilewa na kuijali sayari hiyo. Pamoja na hayo yote kuna tatizo ambalo liko ndani ya wezo wetu  hasa la kuweza kufanya sadaka kwa ajili ya ustawi wa wengine na wa dunia, amebainisha kiongozi huyo.

Kwa mtazamo wa Kiongozi huyo wa Costantinople amesema, Covid  ndiyo kweli imefundisha somo muhimu la kusikiliza na kujifunza kutoka kwa wengine na kuibua uwezo na thamani za upendo na mshikamano. Janga linatukumbusha kuwa ulimwengu ni mkubwa zaidi ya wasiwasi wetu, hamu binafsi,  kanisa letu, na jumuiya ya imani ni mkubwa kuliko uwezo wetu kisiasa na mafao ya kitaifa. Upunguaji wa uchafuzi wakati wa kipindi cha lockdown au karantini, hauwezi kuwa ndiyo maendeleo ya kweli ambayo yanasimika  juu ya uharibifu wa mazingira ya asili.

Patriaki Bartholomew I amejikita aidha katika mzizi wa uhusiano wa athari kati ya ubinadamu, na  wanyama. Siyo bahati mbaya amesema  kuongezeka kwa magonjwa yanayosambazwa na wanyamapori ambapo kumetokea pamoja na uvamizi unaokua wa wanadamu wa ulimwengu wa asili na mabadiliko ya haraka tabianchi. Janga hilo, ameongeza kusema Patriaki Bartholomew I, siyo kitendo cha 'kulipiza kisasi' kwa upande wa Mungu, lakini ni wito zaidi wa  njia ya kuheshima maumbile kwa sisi sote”.

28 January 2021, 16:05