Tafuta

BANGLADESH:WIKI YA MAOMBI KWA AJILI YA UMOJA WA KIKRISTO BANGLADESH:WIKI YA MAOMBI KWA AJILI YA UMOJA WA KIKRISTO  

Bangladesh:Juhudi za Kanisa ili kushinda kutoelewana na chuki

Katka tukio la Wiki ya Kuombea Umoja wa Kikristo kuanzia tarehe 18 hadi 25 Januari,hata Kanisa nchini Bagladesh wanaadhimisha hata katika vikwazo hivi vya janga la kiafya.Kwa upande wa wakristo nchini humo ni hatua moja muhimu ya kiekumene kwani umoja na ushirikiano ni mambo msingi katika Nchi hiyo ambayo wakazi wengi ni waislamu.Lazima mazingumzo yawepo ya kubadilishana mawazo na matendo ya kiroho na kichungaji.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Hata nchini Bangladesh katika Wiki ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo wanaisheherekea kwa namna ya pekee katika vizingiti kutokana na janga la virusi vya corona ambavyoo bado vinatikisa ulimwengu mzima. Mikutano mingi kwa siku nne karibu inafanyika kwa ngazi mahalia na kwa ushiriki wa watu wachache tu, ili kuepuka maambukizi zaidi. Kwa upande wa wakristo nchini Bagladesh ni hatua moja muhimu ya kiekumene kwani umoja na ushirikiano ni mambo msingi katika Nchi hiyo ambayo wakazi wengi ni waislamu kwa mujibu wa Padre Leonardi C. Rebeiro, msimamizi wa Jimbo Kuu Chittagong.  Aidha amesema kwamba nchini Bangladesh sehemu kubwa ya wakristo wanaishi kwa amani na maelewano lakini kati yao lazima kuwepo ushirikiano zaidi. Lazima mazingumzo yawepo zaidi ya kubadilishana mawazo na matendo ya kiroho na kichungaji, kwa namna ya kwamba watu wa imani nyingine wanaweza kutambua kuwa kweli hao ni wafuasi wa Kristo.

Pamoja na hayo yote ya uwepo wa uwazi wa tofauti za mafundisho, lakini bado kuna kutoelewana na kulaumiana, kwa mujibu wa maelezo yake  Padre huyo kwamba mara nyingi wakatoliki wanajifikiria kuwa ni bora zaidi ya waprotestanti. Kwa upande mwingine Padre Rebeiro amesema,lakini hata  waprotestanti na wanawacheka wakristo kama wanaoabudu miungu. Kwa maana hii,  wawe wakatoliki au waprotestanti wanatafuta kuzungukia sheria wakati wa ndoa za mchanganyiko.

Kutokana na maelezo hayo amesema linaongezea tena suala la propaganda kali kwa baadhi ya madhehebu yanayoibuka vijjini kati ya wakatoliki maskini zaidi au wasioelimika na ambao wanasababisha mkanganyiko na mivutano. Kanisa Katoliki nchini Bangladesh linafanya kazi kwa uhai wote ili kuondoa vizingiti hivi kwa njia ya mazungumzo na mipango ya mafunzo ya kidini. Katika siku nane za maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo, Kanisa Katoliki nchini Bangladeshi nao wanatoa mafunzo yaliyoandaliwa mwaka huu na Jumuiya ya kitawa katika Monasteri ya Grandchamp, nchini Uswizi. Ikumbukwe nchini Bangladesh Wakristo wanawakilisha asilimia 0,5 ya watu wote ambapo asilimia 90 ni waislamu, Wakatoliki ndiyo idadi kubwa ya wakristo waliomo nchini huo.

22 January 2021, 10:58