2018.12.28 Familia Takatifu 2018.12.28 Familia Takatifu 

Ureno maaskofu wanasema Familia takatifu ni shule ya fadhila

Kitengo cha Kitaifa cha Huduma ya Kichungaji cha Baraza la Maaskofu nchini Ureno wameandika ujumbe wao na kuusambaza siku ya Dominika tarehe 27 Desmba katika maadhimisho ya Familia Takatifu ya Yesu Maria na Yosefu.Katika ujumbe huo wanabainisha kuwa Familia Takatifu ni shule ya fadhila.Ujumbe wao unaongozwa na kauli mbiu"Mbegu za tumaini”.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Familia Takatifu ni shule ya fadhila ambayo inaishi kwa uaminifu kwa Mungu katika maisha ya kila siku kwa kuonesha wema wa moyo na tumaini ambalo diama ni jipya. Ndivyo wanaandika Kitecho cha kitaifa cha huduma ya Kichungaji ya Familia(Dnpf) cha Baraza la Maaskofu nchini Ureno, katika ujumbe uliosambazwwa katika siku ambayo mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Familia Takatifu, ambayo kama kawaida uadhimishwa kila Dominika ya kwanza baada ya Noeli.

Familia Takatifu inabainisha wazi fursa ya neema na imani

Katika ujumbe wao maaskofu nchini Ureno,  umepewa kauli mbiu “Mbegu za tumaini ambapo  katika Hati hiyo inasisitiza kwamba fadhila za Yesu Yosefu na Maria zinatufanya kutumaini kwa imani na kwamba jumuiya ya kikristo na kibinadamu iweze kujenga juu ya upendo mkarimu, mnyenyekevu na ulio rahisi. Katika matatizo, mahangaiko na kukata tamaa, Familia Takatifu inajionesha wazi kama fursa ya neema na imani, katika kuelewa kwa kina maisha kama utume na kwa ajili ya kukua katika maelewano ya kifamilia. Katika mtazamo huo, Familia ya Nazareth inachangamotisha kiungo cha familia ya sasa kwa kutafuta kuwa na maisha ya amani, huduma, ukarimu, zawadi, kusikiliza wenye kuhitaji zaidi, na ili hatimaye kuweza  kukabiliana na matatizo ya kila siku bila kukimbilia kuwa na mashaka ambayo mara nyingi yanavamia kuta za nyumba nyingi, wanasisitiza maaskofu.

Kila mjumbe wa familia ni tunu msingi kwa ajili ya wengine

Kiukweli kila mjumbe wa familia ni tunu msingi kwa ajili ya wengine, wanaadika kitengo hiki (Dnpf) na kwamba ni jambo la kushangaza, utajiri mkubwa usio na kipimo, kwa maana ili wote waweze kupendana na kufanya maisha yao kuwa zawadi kama walivyofanya Yesu, Yosefu na Maria. Kufuatia na hilo, ndipo wanatoa mwito kwamba katika mikono ya familia nyingi, kuna utume maalum, na ambao uwe wa kukuza uvumilivu na kueneza matumaini na kuwa na moyo mkuu wa uwajibikaji. Hata hivyo Kitengo cha Huduma ya kichungaji ya kifamilia nchini Ureno wanao utambuzi kuwa familia haziwezi kuwa zote kamilifu, walakini, hizo  zenyewe zinaweza kujikamilisha daima na zaidi katika kubadilisha upendo na kutamani utakatifu.

27 December 2020, 11:52