Tafuta

Papa Francisko na Patriaki Sako Papa Francisko na Patriaki Sako  

Ujumbe wa Patriaki Sako kwa wakristo na taifa katika fursa ya hija ya Papa huko Iraq

Katika fursa ya matarajio ya Ziara Kitume ya Papa Francisko kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi 2021,Patriaki Sako amewaandika barua wakristo na watu wote wa Iraq akionesha lengo la ziara ya Papa kuwa ni kwa ajili ya kikanisa na kitaifa hivyo wanapaswa kujiandaa hata kiroho kwa ziara hiyo.Ni imani yake Patriaki kuwa ziara ya matumaini na kutiwa moyo wa ujenzi wa amani na msimamo.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Mara baada ya kutangazwa habari kuhusu matarajio ya Papa Francisko kutaka kwenda ziara ya kitume nchini Iraq kuanza tarehe 5 hadi 8 Machi 2021, Patriaki Raphael Sako ameandika ujumbe kwa wakristo na watu wote nchini humo. Ni ziara kwa upande wake ambayo itaacha ishara kubwa katika Kanisa na nchi kwa ujumla. Papa kupitia nyayo za Baba Ibrahim  ni kwamba hafanyi ziara ya utalii badala yake ni kuwapelekea ujumbe wa amani  na kuwatia moyo na nguvu wote katika kipindi chao kisichokuwa na uhakika.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Kanisa la Wakaldayo, amesema ni ziara ambayo lazima waiandae kikamilifu, kwa namna ya kitaifa, kikanisa na kiroho kwa kuwekea umakini wake. Ni ziara ambaye itawatia moyo watu wa Iraq katika kukabiliana na kuweza kushinda wakati mchungu na kwa ajili ya kujipatanisha na kuponya majereha na wakati huo huo kwa ajili ya kuungana na kusaidiana katika matazamio ya maendeleo ya nchi yao.

Kardinali Sako aidha amesema na zaidi ya imani na msimamo ambao wana uhitaji ili kuweza kuishi kwa pamoja, kuheshimiana katika tofauti za lugha na tamaduni ili wapate kuwa kama ndugu wa kutoka sehemu mbali mbali ,lakini wakiwa ni familia moja ya wazalendo wa ardhi ya Ibrahim, na vile vile Iraq iwe nyumba ya kuishi kwa  pamoja na kwa njia hiyo lazima kuungana!

Akiwageukia wakristo kwa namna ya pekee anasema, ziara hii ni kama fursa ya hija katika mizizi ya kwanza ya kikristo, ya uongofu na ushikiliaji wa uzalendo wao wa wakisto na wa Iraq. Kufuatana na hiyo lazima wawe na uwezo mkuu wa tukio hili bila kuwaacha lipite bila kuwa na ishala yoyote inayobaki ndani mwao katika makanisa yao na nchi yao kwa ujumla.

Kama wajuavyo makanisa yao ya kikaldayo nchini Iraq na makanisa mengine dada nchini Iraq na nchi za Mashariki katika kuishi chini ya ukandamizwaji na changamoto tofauti kama vile, sera za kisasa , kiuchumi na kijamii, kwa sababu ya migogoro ya kivita, ya ugaidi, ya uhamihaji na madhara mengiza zaidi yanayoendelea na Virusi vya Corona, hali halisi zote zimechangamotisha mtazamo na kuleta ugumu wa mahusiano  ya wartu na wa kazi. Lakini lazima kufanya kila liwezekanalo ili katika fursa ya ziara ya Papa inawezekane kubadilisha kila kitu kwa namna ambayo imani na matumaini yanakuwa ndani mwao kama uwajibu na jitihada, anasisitiza Patriaki Sako.

 

11 December 2020, 16:04