Patriaki Pizzaballa amesisitiza msukumo mpya wa kichungaji unaohitajika
Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Patriaki wa Killatino huko Yerusalemu Pierbattista Pizzaballa ambaye tarehe 4 Desemba aliingia rasmi kama Patriaki katika Kanisa la Kaburi Takatifu aliadhimsha misa ya Kipapa huku akistoa shukrani kubwa kwa Mungu. Katika mahubiri yake amesema “Katika Eneo hili Takatifu, linataka kunizawadia nguvu, ujasiri na kutoa maisha yangu katika Kanisa hili, kulipenda na kuelekeza na roho ya ubaba na uvumilivu”. Patriaki mpya mawazo yake yamemudisha nyuma ya mchakato wa safari yake ya utume ambapo, amekumbusha jinsi alivyofika katika Nchi Takatifu miaka 30 iliyopita akiwa kuhani mpya, kuanza mafunzo yake na hatimaye huduma yake ya kichungaji kama Msimamzi wa Nchi Takatifu ambayo imempa fursa ya kutambua zaidi na zaidi Kanisa la Yerusalemu.
“Sisi tunatembea pamoja na Mungu ambaye tunamjua, lakini ni katika kuelekea wakati ujao tusioujua amesisitiza Patriaki Pizzaballa huku akitazama hasa kuhusu kipindi cha sasa, kwani wakati wetu ujao ni wenye mashaka na ambao unaweza kusababisha janga, ambalo lonaendelea, hofu na hisia mbaya. Kwa maana hiyo amesema ni lazima kujikabidhi kwa Mungu anayetambuliwa na ambaye alijifunua wazi kupitia mwanayeYesu ili kupata faraja na nguvu. Lazima kuwa na matumaini na imani ya mioyo yetu ikumbuke historia ya pamoja na ya kila mmoja binafsi na kukumbuka mara ngapi tumewza kufanya uzoefu wa uaminifu wa Mungu kwetu sisi, amekazia Patriaki mpya.
Akiendelea na mahubiri yake ameshauri kujikabidhi hata katika Neno la Mungu, kama Petro akiwa katika ziwa la Tiberiade, ambapo kwa hakika hakuficha hisia zake za hofu mbele ya utume wake aliokabidhiwa hivi karibuni na Papa kuongoza Upatriaki wa Kilatino wa Yerusalemu.Kwa maneno yake kuhusu utume huo amesema “ Ninakubali kwa utiii utume huu ambao ninapendelea kuupeleka mbele kwa furaha”. Hakika pia ni Msalaba, lakini Msalaba huzaa matunda ya wokovu kila wakati unapokaribishwa kwa furaha ” Amesisitiza. Akiongelea juu ya Kanisa la Yerusalemu, Patriaki huyo amebainisha kwamba msukumo mpya wa kichungaji unahitajika, na ambao unazingatia maeneo yote na tamaduni tofauti, lakini ambayo inatambua jinsi ya kutafuta na kupata umoja kati ya wote na kwamba kuna shida za kiuchumi na kijamii ambazo zinatakiwa kushughulikiwa, zilizozidishwa na zaidi na janga linaloendelea.
“Tunasubiriwa kufanya mkutano na Makanisa mengine dada na ndugu Waislam na Wayahudi ambapo pia tunasibiri kupata hata neno la wazi na lenye utulivu kutoka siasa ambalo mara nyingi ni dhaifu la muda mfupi”, amesema Patriaki Pizzaballa. Kwa maana hiyo Patriaki ameomba waamini kusali kwa ajili ya utume wake na kwa ajili ya Kanisa la Yerusalemu, na akahitimisha mahubiri yake amesema “ tunao uhakika kwamba Mfufuka arambua kwa namna nyingine kutjaza Roho wake na kutufanya kuwa katika Nchi yake Mashuhuda wa kweli wa upendo wake.”