Kardinali Bassetti Kardinali Bassetti 

Italia:Kipindi cha Noeli 2020 ni fursa ya kuamini thamani za kweli!

Noeli ni kipindi cha kuamini na kuipa thamani kile ambacho kinastahili katika maisha ya kila siku.Ni ushuhuda wa Rais wa Baraza la Maaskofu Kardinali Bassetti akikimbuka siku ambazo amelazwa akiwa na maambukizi ya covid-19 siku chache zilizopita.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Haijawahi kutokea kama leo hii  licha ya kuwa katikati ya matatizo na mateso na katika hali kama hii kuwa  kupindi cha kuamini na kutumainia. Mwaka huu kiukweli tunaadhimisha tumaini lililofanyika katika mwili kwa unyenyekevundani pango la Betlhehemu na  kukatisha katika dunia. Ndivyo anaandika Kardinali Gualtiero Bassetti, Askofu Mkuu wa Perugia na Rais wa Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Italia katika taariri yake kwenye gazeti la ‘Avvenire’ la Baraza la Maaskofu  nchini Italia.  “Janga utafikiri linatak kukatisha kila mantiki ya maisha, lakini Mwokozi anaendelea kuzaliwa kwa ajili yetu na ndani mwetu. Mungu hatuachi peke yetu. Ninaamini na kuwa uzoefu wa ugonjwa ambao hata mimi nimekabiliana nao na ninaendelea kuushinda kwa neema ya Mungu, kwa maana hiyo imani unaturihisishia kuipa ile thamani kwa kile ambacho ni muhimu.” Anaandika Kardinali Kardinali Bassetti aidha anathibitisha kuwa:“Kwa kutafakari juu ya tukio hili, kwa kuzaliwa kwa Bwana tunaulizwa swali la kina na kuturudisha juu ya jambo la msingi katika maisha yaani kile chenye maana ya kila siku, katika uzuri wa maisha ya familia, uzuri wa uhusiano, uwezo wa kukarimu na kukaribisha Kristo mioyoni mwetu”. Akikumbuka watu waliokufa kutokana na covid-19, waliobaki na upweke, waliopoteza kazi na ambao wanaishi katika hali ya kukatisha tamaa, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia amethibitisha kuwa “mateso haya yasiyo na hatia, yatutafakarisha na kutusaidia kutafakari kuhusu zawadi ya maisha. Sasa ni kipindi muafaka kwa kila mmoja kuwa na jitihada si tu kulinda maisha tuliyopokea kutoka kwa Baba bure, lakini pia hata kuweza kuyatoa”. Katika taariri hiyo anahitimishwa kwa kuwatakia heri ya siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana wale wanaoteseka, wagonjwa, walio na upweke, wazee, madaktari, wahudumu wote wa afya, familia, watoto, vijana na wale wote ambao wanahagaika kutafuta ajira, wanaume na wanawake wote ambao wanatoa kwa ukarimu.

Na matumaini ni zawadi ya Mungu ni uhakika wa ahadi za Mungu kutimilizika

Gualtiero Bassetti, Askofu Mkuu wa Perugia na Rais wa Baraza la la maaskofu Italia, katika ujumbe wake wa matashi mema ya Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana aliyo wakabidhi mitandao ya kijamii ya jimbo amejikita juu ya tumaini kubwa katika Mungu huku akionesha kumbu kumbu ya kulazwa kwake kutokana na kuambukizwa na Covid-19 mwezi Novemba.  Hatua za ugonjwa alizokuwa anaamini kwamba anakabidhi roho yake kwa Bwana na nguvu hiyo imefufuka na sauti awatakiayo kuwa na ujasiri.  Kardinali ameeleza kile kiitwacho jambo la kutisha, akiwa na maana ya upweke kwani amethibitisha kuwa: “Nilikuwa ninasikia mara nyingi wanasema kufa kiupweke ni jambo lisilo elezeka na kwani nimehisi uzoefu huo lakini sikuwa naogopa kwa maana ya kujikabidhi kwa Bwana”. Hata hivyo amesema katika kipindi cha mateso kwa wote hatuwezi lakini kuacha ujumbe ambao unaoneshwa na Noeli, siku ambayo kweli matumaini yanazaliwa kwa upya ili kujitazama binafsi na kuweza kuwatazama wengine. Ni siku ambayo tunapaswa kuwa wakweli kwa Mungu, binafsi na kwa ulimwengu.  Hii ni kwa sababu hakuna lolote katika kuzungumza kibinadamu, kuwa jambo rahisi na la kushangaza la mtoto ambaye anazaliwa katika pango ili aokoe ubinadamu wote. Kardinali Bassetti aidha amewakumbuka wote ambao wanafanya kazi kwa ajili ya kuwasaidia wengine na kufananisha ugonjwa wa covid kama jangwa, kwa sababu linaondoa nguvu zote za maisha na kwa hakika inakuwa vigumu kujenga kwa upya kwa hara hata kimwili na maisha binafsi. Kwa maana hiyo inahitaji ujasiri.  Kwa wale wote ambao kwa sasa wanaendelea kuteseka Kardinali anaungana nao katika mateso na kuwatia moyo na kwamba yupo mtu ambaye yuko karibu nao, kuna mtu ambaye amekuja kwa ajili yao. Matumaini siyo jambo ambalo linapelekea udanganyifu ili kushinda vipindi vya huzuni.Matumaini ni zawadi ya Mungu, ni uhakika kuwa ahadi za Mungu zinatimilizika.

25 December 2020, 11:41