Utetezi wa watoto waathirika Utetezi wa watoto waathirika 

Ripoti kuhusu McCarrick,Maaskofu wa Marekani wana uchungu kwa waathirika!

Askofu Mkuu wa Los Angeles José H.Gomez,Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Marekani anasema Hati ya Ofisi ya Katibu Vatican kuhusu aliyekuwa Kardinali inathibitisha juu ya kuendelea kupambana kwa ajili ya uongofu wa mioyo yetu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Askofu Mkuu wa Los Angeles José H. Gomez ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Marekani, katika kutoa maoni yake juu ya Ripoti ya utambuzi wa Kitaasisi na uamuzi wa mchakato wa Vatican, unamhusu aliyekuwa Kardinali Theodore Edgar McCarrick amendika kuwa: “Kwa waathirika wa McCarrick na familia zao na kila mwathirika chini ya manyanyaso ya kijinsia kwa upande wa Uklero, ninaelezea uchungu wangu wa kina na samahani ya kina”.

Hii kwa mujibu wa Askofu Mkuu Gomez ni janga jingine latika sura ya mapambano marefu ya Kanisa ili kukabiliana na uhalifu wa manyanyaso ya kijinisia yaliyotendwa na klero. “Mimi na ndugu zangu maaskofu tupo katika jitihada za kufanya kile kiwezekanacho ambacho ni uwezo wetu wa kuwasaidia kwenda mbele na kuhakikisha kuwa hakuna nayeteseka kwa kile ambacho mlilazimika kuteseka”.

Ushauri unatolewa kwa wote ambao walipata manyanyaso kwa upande wa kuhani, Askofu au yoyote yule wa Kanisa ni kuripoti uhalifu kama huo kwa polisi na viongozi wa Kanisa. Askofu wa Los Angeles anakumbusha zaidi kwamba habari juu ya jinsi na wapi kuripoti visa vya unyanyasaji pia inaweza kupatikana kwenye ukurasa wao kwenye tovuti ya Baraza la Maaskofu Marekani. Ripoti ya McCarrick, anakumbusha kuwa inasisitizia juu ya ulazima wa kuomba toba na kukuza jitihada za kuhudumia watu wa Mungu. “Sisi sote tunaendelea kuomba na kupigania uongofu wa mioyo yetu na kumfuata Yesu Kristo kwa uadilifu na unyenyekevu”.

11 November 2020, 17:51