Nchi Takatifu Nchi Takatifu 

Ratiba ya siku kuu zijazo za liturujia Nchi Takatifu!

Ili kuweza kufuatilia maisha ya liturujia katika usimamizi wa nchi Takatifu,Shirika la Ndugu wadogo wafransikani(OFM)huko Yerusalem wametoa ratiba ya maadhimisho yao kupitia mtandao,kwa ajili ya kushirikisha kila mmoja anayetaka kuungana nao moja kwa moja katika maadhimisho hayo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumuiya ya usimamizi wa nchi Takatifu ambao ni Ndugu Wadogo Wafransikani (OFM)wametangaza ratiba ya maadhimisho ya Liturujia kwa mwaka 2021 kuanzia na zile za sikukuu muhimu. Kalenda hiyo ya kilatino inapatikana katika Tovuti ya Jumuiya ya kifransikani ya Usimamizi w anchi Takatifu, lakini pia kwa ajili ya wale ambao wanataka kushiriki moja kwa moja maadhimisho ya kifransikani na Nchi Takatifu. Ratiba hiyo inafuata mwaka wa kiliturujia kuanzia na Dominika ya kwanza ya Majilio ambayo mwaka huu inaangukia katika Dominika, tarehe 29 Novemba 2020 na ambayo wanabainisha kwamba ni tarehe mbayo inakumbusha kuingia rasmi kwa wafransikani kama wasimamizi wa Nchi Takatifu huko Betlehemu.

Kwa mujibu wa maelezo yao ni kwamba ni njia ya kutoa fursa ya kufuatilia moja kwa moja maisha ya kiliturujia ya wafransiskani katika Jumuiya yao kwenye Nchi Takatifu kwa wale wote wanaopenda na wanaotaka kusali pamoja na Wafransiskani kama wasimamizi wa maeneo matakatifu, lakini kufuata hija ambazo kwa kipindi chote cha mwaka zinaashiria kumbu kumbu na kujitoa katika maeneo ambayo yaligusa maisha ya dunia ya Bwana Wetu Yesu Kristo.

Pamoja na ratiba hiyo ya kiliturujia, wameonesha hata Hija na Liturujia kwa lugha ya Kiitaliano, Kiingereza na Kispanyola na maelekezo ya sherehe maalum. Na kwa maana hiyo mnamo tarehe 5 Januari 2021, huko Bethlehemu, kutakuwa na afla ya kuingia Msimamimizi wa nchi Takatifu, Padre Francesco Patton, saa 5.30 majira ya asubuhi na ikifuatiwa na Masifu ya kwanza ya jioni na maandamano. Wakati tarehe 6 Januari 2021 katika siku kuu ya Tokeo la Bwana au (Epifania), Misa imepangwa kuadhimishwa   saa 4.00 asubuhi.

Pia katika mwezi wa Januari, tarehe 10, ni siku ambayo itakuwa ya ubatizo wa Yesu, misa itaadhimishwa, saa 3.00 asubuhi itakayoongozwa na Padre Patton, baadaye kwenda Yeriko na saa 3.45 asubuhi msafara na Misa ukingoni mwa mto Yordani. Aidha mnamo tarehe 17 Januari 2021 Misa itaadhimishwa huko Kana katika kukumbuka maadhimisho ya muujiza wa kwanza wa Yesu.

09 November 2020, 14:47