2019.11.22 Ziara ya kitume ya Papa Francisko huko  Thailand na Japan: Misa na Vijana katika Kanisa Kuu la Maria Mpalizwa mbinguni, Bangkok 2019.11.22 Ziara ya kitume ya Papa Francisko huko Thailand na Japan: Misa na Vijana katika Kanisa Kuu la Maria Mpalizwa mbinguni, Bangkok 

Kanisa Kuu la Bangkok waadhimisha mwaka mmoja tangu ziara ya Papa Francisko!

Maelfu ya waamini wakatoliki wameshiriki Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la la Bangkok iliyoongozwa na Kardinali Xavier Kriengsak Kovithavanij,Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Thailand na Askofu Mkuu wa Mji Mkuu wa nchi hiyo kukumbuka mwaka mmoja tangu Papa Francisko afanye ziara ya kitume kunako Novemba 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika fursa ya mwa wa kwanza wa ziara ya kitume ya Papa Francisko huko Kaskazini mwa bara la Asia na uziduiz wa mwaka wa vijana katoliki nchini Thailand, maelfu ya waamini  katoliki wameshiriki Jumapili tarehe 22 Novemba katika maadhimisho ya Misa takatifu katika Kanisa kuu la Maria mpalizwa la Bangkok, kwa kuongozwa na Kardinali Francis Xavier Kriengsak Kovithavanij, na Rais wa Baraza la maaskofu katoliki la thailandese na Askofu Mkuu wa  Bangkok.

Umefikia wakati na maana ya kwamba Baraza la Maaskofu wa Thailand wameweza kuunganishwa leo hii pamoja ili kuadhimisha mwaka wa vijana katoliki nchini Thailand na kuonesha kwa mara nyingine tena ujumbe wa Papa kwa vijana wote ambao tunawapenda na ambao tunawatakia kila mema na baraka”, amesema Kardinali. Muwe na uhakika wa kuwa waakti uliopo na wakati ujao wa Kanisa na jamii ya Thailand amebainisha huku akiongeza kusema kuwa “tunawatakia vijana wote waishi maisha yao katika roho ya kikirsto, kwa mujibu wa ujumbe uliotolewa na Baba Mtakatifu kwa wote wakati wa mahubiri yake na kufuata mfano wake na matendo yake”.

Papa Francisko alitembelea nchini Thailand kuanzia tafehe 20 hadi 23 Novemba 2019. Ilikuwa ni ziara yake ya Pili ya Papa kutembelea nchi hiyo baaa ya ile ya Mtakatfu Yohane Paulo II kunako mwaka 1984. Alitembelea nchi ka kuongozwa na kauli mbiu “ Wafuasi wa Kristo, wafuasi wa kimisionari” ziara amvayo ilifanyika katika fursa ya kumbu kumbu ya miaka 350  tangu usep wa Makao ya kitume ya Siam, iliyoinuliwa kunako mwaka 1669, ambao ulikuwa ndiyo mwanzo wa uwepo wa Kanisa nchini Thailand.

Wakati wa maadhimisho Kardinali  Kriengsak alishirikisha waamini juu ya uzoefu wa kukutana na Papa. “ Niliona mwendendo wake, yeye ni Habari Njema ambayo alileta furaha kwa wale wote waliokutana naye. Baba Myakatifu anajua namana ya kuzungumza na watoto na vijana na kutembea nao pamoja katika muungano na yule wa kuwa na imani katika Kristo aliye hai katikati yetu na ambaye alitìuisha moyo wa ujana. Karibu waamini katoliki 400.000 wa Thailand wanawakilisha karibia asilimia 0,5% ya wakazi milioni 65 katika nchi.

 

24 November 2020, 15:36