Tafuta

2020.06.26  ulemavu wa viziwi na vipofu 2020.06.26 ulemavu wa viziwi na vipofu 

Ghana:Uzinduzi wa utume kwa ajili ya viziwi ili kushinda ubaguzi&kutengwa!

Ili kushinda kutengwa na ubaguzi ambao viziwi na vipofu wanakabiliwa ndilo lengo la Jumuiya ya Shirika la Utume wa Afrika (SMA) nchini Ghana ambao wamezindua ukiwa wa kwanza nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Watu viziwi wamewekwa kwa muda mrefu pembeni kwa maaa hiyo kuna haja ya wao kupokea sakrametni ya ubatizo na ili waweze nao kuudhuria katekisimu au kufuatiliwa katika maandalizi ya kupata kipaimara na kufunga ndoa. Ni kwa mujibu wa Padre René Dan Yao msimamizi wa utume mpya kwa ajili ya viziwi iliozinduliwa nchini Ghana na Shirika wa wamisionari wa utume wa Afrika (SMA).

Shughuli hii imezinduliwa tarehe 22 Novemba 2020 sambamba na sherehe za miaka 140 tangu uwepo wa shirika hili nchini Ghana. Kwa mujibu wa Padre Yao amesisitiza kuwa ni namna ya kuendeleza kazi ya uinjilishaji ulioanzishwa miaka mingi iliyopita, na ili kuonesha kuwa bado ni hai na inaendelea hasa kwa ajili ya watu wenye kuhitaji zaidi na katika mazingira magumu.

Siyo kwa bahati mbaya msimamizi wa utume huo mpya wamechagua Mtakatifu Martino wa Porres, ambaye alitambua kwenda kukutana na mahitaji ya walio na mazingira magumu zaidi. Wakati huo huo Padre René amesisitiza umuhimu wa kukuunda utume huo kwa utambuzui zaidi ndani ya Kanisa la Ghana , na juu ya hali halisi ya waamni ambao wanaishi na ulemavu huo wa uziwi. Lengo la kwanza la utume huo mpya utakuwa ni kutoa umakini kwa watu viziwi na mahitaji yao ya lazima katika huduma. Hatua ya pili itakuwa ni kuongeza watu kujifunza njia za kutumia lugha ya ishara.

28 November 2020, 14:31