2020.10.09 Kambi ya wahamiaji nchini Sudan Kusini  2020.10.09 Kambi ya wahamiaji nchini Sudan Kusini  

Sudan Kusini:Viongozi wa Makanisa waomba msaada wa kibinadamu!

Sudan Kusini,ni nchi dogo zaidi ulimwenguni na ni kati ya mataifa yaliyogawanyika zaidi katika Afrika ya Kati.Tangu 2013 wanateseka na vita ya wenyewe kwa wenyewe.Baraza la Makanisa nchini humo wamezindua wito wakiomba msaada wa kibinadamu kwa watu ambao wanaishi kipindi kigumu kilichotokana na dharura ya virusi vya corona,ukosefu wa usalama wa chakula,uvamizi wa nzige na mafuriko.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baraza la Makanisa nchini Sudan kusini (Sscc) wamezindua wito ili kuweza kuhakikisha wanapata msaada wa kibinadamu kwa watu wa nchi ambao wanaishi kipindi  kigumu kilichotokana na dharura ya virusi vya corona, ukosefu mbaya sana wa usalama wa chakula, uvamizi wa nzige, mafuriko makali vile vile na matokeo  ya madhara mengine mengi yaliyosababishwa na vita ya miaka sasa, tangu 2013. Ni kwa mujibu wa Baraza la Kiukemene la Makanisa (Coe) katika hati yao iliyotiwa saini na viogzoi wa kidini, miongoni mwake ni Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin Mulla, wa Jimbo Kuu la Juba ambao wanaomba Makanisa la Kiekumene ulimwenguni, Jumuiya zote za imani, wafadhili wa kimataifa, mashirika binafsi na marafiki, kuingilia kati ili kusaidia jumuiya hii iliyoko kwenye matitizo makubwa.

Sudan Kusini, ni nchi dogo zaidi ulimwenguni, kati ya mataifa yaliyogawanyika zaidi katika Afrika ya Kati na zaidi ya makabila 60 ya dini tofauti, inajaribu kumaliza mzozo wa kikabila ulioibuka mnamo Desemba 2013 kati ya wanajeshi watiifu wa Rais Salva Kiir Mayardit, kabila la Dinka, na wale wanaohusishwa na makamu wa rais wa zamani Riek Machar, kabila la Nuer, ambao wanatuhumiwa kuandaa mapinduzi. Tangu wakati huo, kumekuwa na zaidi ya milioni moja na nusu ya wakimbizi wa ndani na karibu watu milioni 7.5 wanaohitaji msaada wa kibinadamu, kati ya idadi ya zaidi ya watu milioni 11. Kwa kuongezea, inakadiriwa kuwa karibu nusu ya idadi ya watu wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na watoto karibu 300,000 wagonja na  utapiamlo. Taarifa ya Baraza la Makanisa la Sudan Kusini pia linaelezea kuwa janga hilo pia limedhoofisha ugawaji, na kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula msingi na malighafi.

Viongozo wa Makanisa wanakaridiria kuwa inahitajika dola za Kimarekani 5000 ili kukidhi mahitaji ya haraka ya watu 100,000 huko Jonglei, Maziwa, Upper Nile, Ikweta na Umoja, ili kuhakikisha upatikanaji wa maji, chakula, usafi wa mazingira, makazi, maisha mema na msaada wa kisaikolojia. Katika miezi ya hivi karibuni, pamoja na mambo mengine, mafuriko ya Mto Nile yameharibu mashamba, yamefuta makazi na shule na takriban watu 700,000 wamehama makazi yao. Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, karibu dola milioni 80 zinahitajika kukabiliana na uharibifu, na dola milioni 46 kwa msaada wa haraka kwa watu 360,000 hadi mwisho wa mwaka. Lakini mzozo unaoendelea na vurugu za kijamii, pamoja na vizuizi vilivyowekwa na janga hilo, vimekwamisha misaada na barabara mbovu zimefanya isiwezekane kwa mashirika ya misaada kufikia maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko. Kwa wakati huu, Baraza la Makanisa la Sudan Kusini, Muungano wa ACT na Caritas wanajaribu kutoa jibu kwa wakati unaofaa kwa dharura.

04 November 2020, 18:10