Tafuta

Vatican News
Mabadiliko ya tabianchi.Ongezeko la joto katika sayari na matokeo yake mabaya. Mabadiliko ya tabianchi.Ongezeko la joto katika sayari na matokeo yake mabaya. 

Cop-26:Wito wa Viongozi wa Kidini kwa serikali ya Uingereza ili iwe mfano

Katika barua kwa Waziri Mkuu wa Uingereza,Viongozi wa Kidini wanaomba serikali iwe mstari wa mbele katika mapambano dhini ya tabianchi wakati wa kuelekea kwenye mkutano wa Cop-26 unatozamiwa kufanyika huko Glasgow,Scotland mwezi novemba 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Itakuwa ni jiji la Glasgow, nchini Scotland kuwa mgeni wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabiachi (Cop-26), unaotarajiwa kufanyika mnamo Novemba 2021. Katika matarajio ya kuudhuriwa, viongozi 60 wa kikristo, wayahudi, waislam, wahindu na Wasikh,  wa Uingereza  wameandika barua ya pamoja kwa Waziri Mkuu Bwana Boris Johnson ili Serikali iandae kuanzia sasa, mpango mzuri wa kitaifa kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi dhidi ya ongezeko la joto katika Sayari. “Kama rais wa sasa wa Cop26, jukumu muhimu zaidi la Uingereza ni kuleta nchi zote pamoja ili kuzungukia malengo ya hali ya hewa ya kutamani zaidi”, imessisitiza barua, iliyosainiwa, kwa niaba ya maaskofu Katoliki na Askofu John Arnold, anayehusika na mazingira wa Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Walles (CBCEW).

Barua hiyo inasisitiza uwajibikaji wa maadili ya kujitoa, ikionyesha athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi kwa wanadamu wote na hasa kwa maskini ambao tayari wanateseka. “Lazima sote tujaribu kuwa na ujasiri wa kimaadili ili kujibu changamoto hii ambayo inatia shaka uhusiano wetu na ulimwengu ulio hai na kutugeuza sisi wenyewe na jamii yetu”. Wameandika viongozi wa dini, ambao wanakumbuka jinsi jamuiya za kiimani nchini Uingereza tayari wanachukua hatua madhubuti  huku maelfu ya maeneo ya ibada wakibadilisha nishati mbadala na vikundi vya kidini vikigawanya mafuta na kuwekeza tena katika hatua za mazingira. Jitihada inayohusishwa na juhudi katika kiwango cha ulimwengu, pamoja ndiyo wito wa haraka wa Baba Mtakatifu Francisko kwa serikali ili kuweka malengo muhimu zaidi mbele ya Mkutano huo COP26 na kazi ya kuongeza uelewa juu ya suala hili na Patriaki wa kiekumene Bartholomew I.

09 November 2020, 14:33