2019.10.31 (CNBB):Marais Askofu Mkuu Walmor Oliveira de Azevedo; na Makamu wake Aksofu  Jaime Spengler 2019.10.31 (CNBB):Marais Askofu Mkuu Walmor Oliveira de Azevedo; na Makamu wake Aksofu Jaime Spengler  

Brazil:Rais wa Maaskofu wa Brazil atoa mwaliko wa kupanda mti katika kumbukizi la marehemu wao!

Katika kuwakumbuka waamini waliotangulia katika mbele ya haki tarehe 2 Novemba 2020,Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Brazil,Askofu Mkuu Walmor Oliveira de Azevedo wa Belo Horizonte amewaomba waamini wote kupanda mti karibu na nyumbani au katika jumuiya kwa ajili ya ishara ndogo ya kuwakumbuka wapendwa wao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mwaliko wa Askofu Mkuu Walmor Oliveira de Azevedo wa Belo Horizonte na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Brazil (CNBB), ambaye kwa ujumbe wake kupitia Video kwa waamini wote amesema “Tupande mti kwa ajili ya kukumbuka marehemu na kwa  namna ya pekee wale ambao wametuacha kwa sababu ya covid. Hii ni ishara ndogo kama Kanisa kwa ajili ya nchi nzima. “Tunaalikwa kushuhudia matumaini yetu  kwa kukabiliana na kifo kwa ishara za upendo”.

Akiekendelea na ujumbe :“Kwa maana hii tunabadilisha maisha tukikabilianaa na kifo”. Akizungumzia  juu ya janga hilo  na maelfu ya watu waliopotea kwa sababu ya virusi vya corona,  Rais wa Baraza la Maaskofu ameelezea mshikamano wake na kuelezea ukaribu wake kwa familia za wahanga hao “Tunashiriki maumivu ya yatima, wajane na kaka  na dada ambao wamekabiliwa na maumivu ya kutengana na kutoweka kwa sababu ya ugonjwa huu”. Akitoa neno kwa Ndugu Wote, askofu Mkuu amesisitiza  kwamba “Mshikamano na uwajibikaji wa pamoja ni sehemu ya utambulisho wa Kikristo. Baba Mtakatifu Francisko anarudia hili  mara kwa mara na katika maandishi yake ya hivi karibuni katika Waraka wa ‘Fratelli tutti’, yaani ‘Wote ni ndugu’  ambao ni kuonesha kweli kanuni kuu ya imani yetu”.

Hatimaye Askofu Mkuu ametoa wito kuwa: Siku hii tunapotafakari juu ya kifo, hatupotezi njia yetu: tumezaliwa katika maisha yote. Tuko kwenye huduma ya kwa hakika kwamba siku moja tutakutana na wale waliotutangulia.  Na kwa kukumbuka suuala la wote ni ndugu amesisitiza kwamba kutoka uthibitisho huo , kwa heshima kwa wahanga wa janga hilo na kukumbuka majanga ya kimazingira yaliyotokea mwaka huu, Kanisa linawaalikoa  tufanye ishara thabiti: upandaji wa mti nyumbani kwako au katika jamuiya yako kwa kumbukumbu ya wale ambao wametuacha”.

02 November 2020, 09:55