Mashambulizi ya kigaidi jijini Vienna nchini Austria Mashambulizi ya kigaidi jijini Vienna nchini Austria 

Austria-Vienna:Kard.Schönborn aomba kusali kwa ajili ya waathiriwa!

Kardinali Schönborn Askofu Mkuu wa Vienne nchini Austria ameomba kuwaombea waathiriwa na na watoa huduma ya dharura kutokana na shambulio lililotokea nchini humo,Jumatatu jioni tarehe 2 Novemba 2020 kwa kusababisha vifo na majeruhi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila aina ya kianzio cha shambulizi lazima kuwa wazi kuwa vurugu zisizofahamika haziwezi kuhesabiwa haki na wala chochote.  Haya ni maneno ya askofu mkuu wa mji mkuu wa Austria, Kardinali Christoph Schönborn, aliyotoa tarehe 3 Novemba 2020 siku moja baada ya tukio la ufyatuaji wa  risasi uliofanyika tarehe 2 Novemba  jioni katika maeneo sita tofauti katikati mwa jiji. Tovuti ya Baraza la Maaskofu wa Austria inaripoti.

Kardinali Schönborn ameomba kuwaombea waathiriwa wa shambulio hilo na kwa watu wote wanaondelea na uotaji wa huduma za dharura: “ Katika masaa haya ya kusisimua, ninaomba na wengine wengi ambao wanafuatilia matukio mabaya katika moyo wa jiji letu kupitia vyombo vya habari, kwa wahanga, huduma za dharura na ili pasiwemo kamwe uwangaji wa damu”, amesisitiza Askofu Mkuu akihojiana shirika la habari la  Kath, ambapo ameeleza tukio hilo  limemgusa kwa kina na matukio ambayo ameweza kushuhudia.

“Ukweli  ni kwamba risasi zilirushwa moja kwa moja mbele ya hekalu la jiji la la jumuiya kidini ya waisraeli, amesema linanikumbusha shambulio la umwagaji damu kwenye sinagogi mnamo 1981. Chochote kile cha msingi wa shambulio kwa wakati huu, ni lazima iwe wazi kuwa vurugu za kipofu haziwezi kuwa haki na chochote”.

03 November 2020, 15:49