Kanisa nchini Australia wanataka kusaidia watoto nchini Ethipia wasio kuwa na fursa ya masomo Kanisa nchini Australia wanataka kusaidia watoto nchini Ethipia wasio kuwa na fursa ya masomo 

Australia:PMS yakusudia kutoa msaada kwa ajili ya mafunzo ya watoto wasio na fursa!

Shirika la shughuli za Kipapa za Kimisionari(PMS)nchini Australia wameanzisha mpango wa kusaidia mafunzo kwa ajili ya watoto wasio kuwa na fursa katika mji mkuu wa Ethiopia.Kusaidia ni kuvunja mzunguko usioisha wa umaskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kusaidia na kuhamasisha mchakato wa mafunzo ya watoto wanaokuja kutoka maeneo ambayo hayana fursa huko Ethiopia, katika nchi ambayo imekumbwa na mivutano ya kikabiliana linalotaharisha hata sasa kuzuka kwa vita vipya, ndiyo lengo la Utume Katoliki  kwa mujibu wa maelekezo ya kitaifa ya shughuli za kipapa za Kimisionariwa Kanisa la  Australia na Kanisa Katoliki la Ethiopia Utume huo unataka kusaidia Shule ya  Kanisa Kuu Katoliki la  Mji mkuu Addis Abeba ambao kwa dhati wameunda mpango kwa ajili ya ufadhili wa mafunzo ili  kuhakikisha watoto ambao ni yatima au wanatoka katika familia masikini waweze kuendelea na mafunzo yaliyo bora na kwa ajili ya kuboresha shule za nchi. Hayo yamesemwa na   S.r Carmen Sammut; SJA, mhusika wa mpango wa ufadhili wa mafunzo ya shule ya  Kanisa Kuu la Adis Abeba, Ethiopia, katika taarifa iliyotolewa na shirika la habari za Kimisionari Fides.

“Mafunzo ya maadili ya shule yana matokeo mazuri kwa wanafunzi na inawasaidia kuwa raia wema, watu waliosoma na tayari hurudisha kwa jamii kile walichopokea kwa maadili na kujitoa kwa faida ya wote” . Amesema hayo Padre Tekle Mekonnen, Mkuu wa Shule ya Kanisa Kuu  Katoliki 'Lideta', aliyejitoa kusaidia watoto wanaohitaji katika jiji la Addis Ababa, anabainisha kwamba : “Tumejitolea kukuza utangazaji wa kibinadamu na wakati huo huo tunakusudia uboreshaji wa kielimu. Tunataka kuwa shule yenye elimu bora na wakati huo huo, ujumuishwaji wa maadili na kanuni za Kikristo. Hili ndilo lengo letu kuu”, amesisitiza Padre . “Familia nyingi zinajitahidi kupambana na umaskini katika hali mbaya ya kiuchumi na kijamii katika mji mkuu wa Ethiopia, lakini kwa sababu ya gharama kubwa ya maisha na nafasi ndogo za kazi wanshindwa. Wazazi wengi hawawezi kulipia gharama za msingi kama masomo kwa watoto wao”.

Utume Katoliki nchini Australia, ambao tayari unatafuta  na kukusudia kuongeza ufahamu kati ya wafadhili  wakati wa Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana  ijayo, itasaidia watoto wasiojiweza kupata elimu katika mwaka ujao wa shule. "Kwa kuungwa mkono wito huo tunaweza kuzifikia familia ambazo zinahitaji na kuwapa watoto udhamini, ili wasikose njia ya elimu, ambayo ni muhimu”, amesema hayo Padri Brian Lucas, Mkurugenzi wa Kitaifa wa Utume Katoliki nchini Australia.

10 November 2020, 16:17