Umakini wa Kanisa la Ujerumani kwa mwezi wa Kimisionari kusaidia nchi za Afrika Magharibi zilizogubikwa na migororo ya aina mbali mbali. Umakini wa Kanisa la Ujerumani kwa mwezi wa Kimisionari kusaidia nchi za Afrika Magharibi zilizogubikwa na migororo ya aina mbali mbali. 

Ujerumani:Siku ya kimisionari:wito wa maaskofu kwa ajili ya Afrika Magharibi!

Mwaka huu umakini wa Kanisa la Ujerumani katika muktadha wa mwezi wa kimisionari ni kwa ajili ya nchi za Afrika ya Magharibi mahali ambapo watu wa dini mbali mbali na makundi ya kikabila kwa miaka mingi waliweza kuishi kwa amani ya muda mrefu sana, lakini kwa sasa, kanda hizi zinagubikwa na migogoro mingi.Kwa njia hiyo Kanisa la Ujerumani limezindua mfuko ili tarehe 25 Oktoba kukusanya fedha kwa ajili ya nchi hizo.

Na Sr.Angella Rwezaula-Vatican.

Heri wahudumu wa amani (Mt 5,9). Ndiyo heri ya Yesu iliyochaguliwa kama kauli mbiu ya mwezi wa kimisionari ulimwenguni 2020 kwa Kanisa la Ujerumani na ambao wamezindua kwa namna ya peeke mfuko wa kukusanya fedha, katika Dominika ya tarehe 25Oktoba ndani ya mwezi huu wa kimisionari kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya Kanisa la Afrika Magharibi. Kwa dhati Kanisa la Ujerumani mwaka huu, ameweka umakini wao ni kwa ajili ya nchi za Afrika ya Magaharibi mahali ambapo watu wa dini mbali mbali na makundi ya makabila waliweza kuishi kwa amani kwa kipindi cha muda mrefu sana.

Kwa bahati mbaya nchi hizi zimegubikwa kuwa uwanja wa mashambulizi na kutumia nguvu. Na huo ndiyo wasiwasi mkubwa unaooneshwa kama mgogoro unaotumia dini kuweka kinzani dhidi ya mwingine na kukuza chochezi za vurugu kwa mujibu wa maandishi ya maaskofu wa Ujerumani na wakati janga la virusi vya corona hali hiyo imezidi kuleta hali mbaya zaidi kwa maisha ya watu wa Mungu. Makanisa ya Afrika Magharibu, kwa namna moja au nyingine wanafanya kazi kwa njia ya kushirikishana kidini ili kupambana kuhusu matumizi ya dini  na kwa kutoa mchango wao wa kuunganisha, na kuleta umoja pale penye kinzani na migogoro kwa njia ya  mazungumzo.

Heri wahudumu wa amani. Katika ulimwengu wa migogoro na machafuko Mungu anaita na nawapatia watu ule uwezo wa kuwa wahudumu wa amani, maaskofu wanaandikia na kuongeza kusema “tunawaomba kuonesha ishara ya Dominika ya kimisionari ulimwenguni. Salini kwa ajili ya dada na kaka zetu wanaofanya kazi kwa moyo wote kwa ajili ya amani na mapatano! Wanaomba maaskofu ili kusaidia mpango wao muhimu wa utume wa kimisionari katika ukusanyaji wa fedha siku ya Jumapili iliyopendekezwa. Fedha zitakazopatikana tarehe 25 Oktoba 2020 zitatumwa kwenye Shirika la Kipapa la shughuli za kimisionari katika ofisi yake iliyoko Aquisgrana na Monaco ya Baviera.

16 October 2020, 12:26