2019.10.20 Misa takatifu siku ya kimisinari ulimwenguni 2019.10.20 Misa takatifu siku ya kimisinari ulimwenguni 

Pwani ya Pembe:wito wa Askofu Kouadio kuhusu Unjilishaji kwa watu!

Askofu Marcelin Yao Kouadio wa Jimbo Katoliki la Daloa, Mashariki ya kati Pwani ya Pembe na Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya uinjilishaji na mhusika wa shughuli za kipapa za kimisionari (PMS)katika ujumbe wake wa fursa ya maandishisho ya siku ya Kimisionari ulimwenguni Dominika tarehe 18 Okotba 2020 amesema Kanisa lipo kwa ajili ya kuinjilisha na kwa maana hiyo ni utume wa asili ya Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kanisa lipo kwa ajili ya kuinjilisha na kwa maana hiyo ni utume wa asili ya Mungu. Kanisa zima na watu wake yaani makuhani, watawa, kike na kiume waamini walei wanajikita katika jitihada zao kwenye kambi za kimisionari, kwa mujibu wa Askofu Marcelin Yao Kouadio wa Jimbo Katoliki la Daloa, Mashariki ya kati Pwani ya Pembe na Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya uinjilishaji na  mhusika wa shughuli za kipapa za kimisionari (PMS) katika ujumbe wake alioutoa katika fursa ya maandishisho ya siku ya Kimisionari ulimwenguni Dominika tarehe 18 Oktoba 2020.

Utume hautazami makuhani, watawa au maaskofu tu, wote wanapaswa kujikita katika shughuli nzima kwa mujibu wa Askofu Kouadio, huku akisema kwamba ni roho Mtakatifu ambaye yuko mstari wa mbele katika utume na kwa waaamini wote anayo nguvu ya Roho Mtakatifu katika ubatizo wetu, kipaimara chetu na kutufanya kuwa sisi sote ni wamisionari. Askofu Kouadio aliukabidhi ujumbe wake tarehe 14 Oktoba nje mkutano  wa wakilishi viongozi wa kitaifa PMS uliofanyika katika kituo cha mapokezi cha  kijimbo huko  Daloa.

Wakati wa ziara yake ambayo imejikita katika kuwakilishi wa ripoti ya  shughuli zote za mwaka kwa upande wa PMS, nchini Pwani ya Pembe Askofu Kouadio amempongeza Mkurugenzi wa Kitaifa, Padre Jean Noel Gossou, na timu yake yote kwa kazi yao wanayojikita nayo, na ameshauri waendelee na shughuli hiyo kwa kutazama hasa matatizo ambayo yameoneshwa na Mkurugenzi wa kitaifa miongoni ma hayo ni  ukosefu wa uelewa zaidi kuhusu shughuli za  Kipapa za Kimisionari kwa upande wa waamini nchini humo. Na kwa maana huyo Askofu Kouadio ameshauri uongozi wa kitaifa wa PMS kujitahidi kukuza matendo yao hasa katika nyanja ya kuhamasisha, mafunzo na kuendeleza mipango ya mawasiliano na  Umoja wa udugu wa uklero wa Pwani ya Pembe (UFRACI), Jumuiya ndogo ndogo za Kanisa (CEB),na makundi mablimbali ya sala.

17 October 2020, 15:00