2020.10.12 Tunza usafi. Endeleza ukijani vijana na mazingira nchini Papua Guinea Mpya. 2020.10.12 Tunza usafi. Endeleza ukijani vijana na mazingira nchini Papua Guinea Mpya. 

Papua Guinea mpya:Tamasha la Kimataifa la Filamu Fupi (ISFF20)kuleta vijana karibu na masuala ya mazingira!

Tamasha la Kimataifa la Filamu Fupi(ISFF20)lililoitwa:“tunza Usafi.Nenda katika Ukijani”ambalo lilifanyika Jumamosi tarehe 10 Oktoba 2020 huko Waigani,Port Moresby nchini Papua Guinea Mpya liliwakilisha hakiki za kazi za kuongeza uelewa wa masuala ya mazingira kwa wanafunzi wa shule na vyuo vikuu vya nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tamasha la Kimataifa la Filamu Fupi (ISFF20), lililoitwa “tunza  Usafi. Nenda katika Ukijani” ambalo lilifanyika Jumamosi tarehe 10 Oktoba 2020 huko Waigani, Port Moresby nchini Papua Guinea Mpya liliwakilisha hakiki za kazi za kuongeza uelewa wa masuala ya mazingira kwa wanafunzi wa shule na vyuo vikuu vya nchi hiyo. Tukio hilo liliandaliwa na Tume ya Mawasiliano Jamii ya Baraza la Maaskofu nchini humo, kwa ushiriki pamoja na wengine Kardinali John Ribat, MSC, Askofu Mkuu wa Port Moresby, wawakilishi wa Tume Kuu ya Australia, ya Caritas Australia, ya makuhani, watawa na waamini, kwa ujumla walikuwa ni mia ya watu.

“Ninyi ni tegemeo la wakati ujao wa nchi na vijana wengi leo hii wanahitaji mipango inayofanana na ili iwaongoze na kuwapa mafunzo na mwelekeo katika maisha” kwa mjibu wa Kardinali Ribat, akiwapongeza wanafunzi hao kwa kazi yaliyoifanya ya filam fupi na ambayo kwa ufupi imewakilisha uhalisia, wa masuala ya kweli na ya sasa, ambayo watu wengi katika nchi hiyo wanakabiliana nayo.

Kutokana na hali halisi hiyo ndipo amewasahauri wawe na jitihada kubwa ili kuunda mabadiliko chanya katika jamii na kutenda katika mantiki zinazohusiana na mazingira. Kwa upande wa hotuba yao, wanafunzi wamebainisha wazi jinsi uzoefu huo ulivyo wasaidia kukua kiroho na kuona ni jinsi gani athari za uharibifu wa mazingira zinaathiri maisha ya binadamu na kwa maana hiyo kuona umuhimu wa kutunza kazi ya uumbaji kwa dhati, ya kwamba ni kwa wote.

13 October 2020, 14:25