Mali:Mafunzo kwa walimu toleo la pili 2020 limehitimishwa!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Walimu, wakuu wa shule na washauri wamejadiliana kuhusu elimu ya amani katika shule kwa mantiki ya uhusiano wa mtindo wa kuishi bila kutumia nguvu hasa katika sehemu zenye migogoro. Kozi hii imehitimishwa hivi karibuni huko Bamako nchini Mali. Kitengo cha mafunzo ya toleo la pili 2020 na ambacho kinatazama Majimbo ya Kayes, Bamako, Sikasso, kimehusisha hata majimbo ya Mtakatifu San, Mopti na Ségou. Kwa mujibu wa taarifa za Baraza la Maaskofu nchini Mali, huo ni mpango kati ya Kozi zilizoandaliwa kwa ajili ya walimu wa Kitaifa wa Elimu Katoliki ili hatimaye kuhakikisha hupatikanaji wa elimu bora na shukrani kubwa kwa ufadhili wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI).
Kwa kuzingatia kwamba nchi ya Mali kila wakati imekumbwa na vurugu, chuki na sintofahamu, Koundia Joseph Guindo, mhusika wa kitaifa wa Mtaala wa Elimu Katoliki amesema kuwa wanaishi wote bila kuwa na usalama. Nchini Mali inahitaji amani. Watu wa mali lazima waweze kuishi kwa pamoja kwa amani. Wakati wa kozi yao, mbinu ya kufundisha kusoma kwa njia ya mtaala na elimu Msingi pia ilijadiliwa. Washiriki, karibu hamsini, pia walipata fursa ya kushiriki uzoefu wao na kuongeza maarifa yao. Mpango huo unaofadhiliwa na Baraza la Maaskofu Italia (CEI) kwa waalimu wa elimu Katoliki hutoa mafunzo ya miaka mitatu mitatu.