2020.10.12 HIstoria ya  Laudato si'- Malaysia 2020.10.12 HIstoria ya Laudato si'- Malaysia  

Malaysia:Shule katoliki ni zana ya uinjilishaji na maendeleo ya binadamu!

Katika mkutano uliofanyika kati ya Taasisi za Kanisa na Ushirikiano na Serikali,nchini Malaysia,Askofu Mkuu Simon Peter Poh Hoon Seng,wa jimbo katoliki la Kuching,amesisitiza kuwa shule na vituo vyote vya mafunzo vinavyoendeshwa na Kanisa ni sehemu fungamani ya maendeleo ya serikali hasa katika kutoa mafunzo msingi kwa watoto wote na zaidi wa maeneo ya vijijini.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican 

Taasisi katoliki nchini Malaysia ni na tunu msingi wa uinjilishaji, maendeleo ya binadamu na kukua kwa mtu. Amethibitisha hayo Askofu Mkuu Simon Peter Poh Hoon Seng, wa jimbo katoliki la Kuching, akisisitiza kuwa shule na vituo vyote vya mafunzo vinavyoendeshwa na Kanisa, ni sehemu fungamani ya maendeleo ya serikali, kwa kutoa mafunzo msingi kwa watoto  wota na hasa  wa maeneo ya vijijini.

Kwa mujibu wa shirika la habari za kimisionari Fides, Askofu Mkuu Hoon Seng, amesema  Shule na vyuo katoliki vinachangia kukuza na kuongeza nguvu hasa katika jumuiya za vijijini kwa njia ya mafunzo stahiki huko Sarawak na katika sehemu nyingi za nchi hiyo. Kwa  mujibu wake amesema huko Sarawak, katika shirikisho la serikali ya Borneo malaysia, abayo inapatikana  katika pwani ya kaskazini magharibi mwa kisiwa, katika maeneo ya vijijini, watoto wasingepata mafunzo yoyote kama pasipengekuwapo shule za kimisionari. Amesistiza hayo katika hotuba yake hivi karibuni katika mkutano wa wakuu wa  na viongozi wa “shule za kimisionari  na Umoja wa dini  nyingine  (Unifor).

Naye Datuk Amar Douglas Uggah, ambaye ni mhusika wa Umoja wa dini nyingine (Unifor), ameshiriki katika mkutano huo kwa ajili ya kujadili mahitaji ya dharura ya shule. Serikali nchini humo iko katika harakati ya kapanga kuweka mfuko kwa namna ya kwamba shule zinazoendeshwa na Kanisa katoliki ziweze kuboreshwa hasa katika majengo na ubora wa shule za kimisionari katika serikali hiyo. Bwana Uggah ametaja nia ya kuomba waziri mkuu Tan Sri Muhyiddin Yassin fedha. Serikali shirikisho ina baadhi ya fedha ambazo zinalekezwa kwa makundi ya kiislam. Tunanapswa kufanya kwamba shule za wale wasio na fursa yaani za vijijini na ambazo hazia kipato kingenea ziweze kweli usaidiwa kwa kupongeza sana taasisi binafsi kama Kanisa Katoliki na wakaristo wengine ambao wako tayari kufungua taaisis na shule katika vijiji na sehemu zilizo mbali sana na miji.

Shule binafsi zinajitegemea na kufuata mtaala wao, zina uwezo pia wa kutoa mafunzo ya juu kabisa amethibitisha. Kwa sasa zipo shule 127 za kimisionari huko Sarawak ambapo shule za msingi 113 na shule 14 za sekondali ambazo zimeagawanyika katika maeneo ya Kuching, Sibu na  Miri.  Shule za msingi katoliki ni 57, za kianglikani ni 45 na wametodisti 5; wakati shule za sekondari 7 zinaendeshwa na Kanisa Katoliki, 5 kanisa la kianglikani na 2 za kanisa la Kimetoditi. Na zadi na shule za awali 92 zinaendeshwa na makanisa hayo madhehebu hayo matatu. Sarawak ni shirikisho la kubwa sana la Malaysia na linapakana na Borneo na kufunika eneo karibu la Peninsula ya Malaysia.

Mji Mkuu, Kuching, ni mji kubwa wa Sarawak na ambao ni kituo kikuu cha kibiashara na  kiuchumi cha serikali na makao makuu ya serikali. Ni serikali iliyo na mchanganyiko wa makabila, utamaduni, lugha, na dini mbali mbali. Makundi ua makabila msingi ni  Iban, Malay, Wachina, Melanau, Bidayuh na  Orang Ulu. Wakazi wa  Sarawak  ni milioni  2,6 (kwa mujibu sensa ya 2015). Sarawak ni mojawapo ya serikali ya Malaysia, mahalia ambapo wakristo ni wengi zaidi kwa asilimia  (42,6%) ya waislam kwa asilimia (32,2%).  Jumuiya nyingine za kidini zilizopo ni wabudha, wahindu , na tamaduni nyingine au za mila. Shirikisho la Malaysia ni nchi yenye makabila mwengi, utamaduni mwengi na dini nyingi. Wakati wake wote ni karibu watu milioni 32,7 na asilimia  60% ni waislamu.

17 October 2020, 15:15