2020.10.16 Nembo ya Siku ya Vijana  lisbon 2023 2020.10.16 Nembo ya Siku ya Vijana lisbon 2023  

Imetolewa Nembo ya Siku ya vijana 2023 huko Lisbon Ureno

Mchoraji wake ni kijana wa Ureno.Alama hiyo in rangi za bendera ya kitaifa,inayonesha msalaba mkubwa katikati kuna rosari na Bikira Maria wakati wa ziara yake kwenda kwa Elizabeti,kulingana na kauli mbiu iliyochaguliwa na Papa kuongoza Siku hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kama ilivyokuwa imetolewa taarifa kuhusu maandalizi ya Siku ya vijana, tarehe 16 Oktoba 2020 imewakilishwa Nembo ya kuongoza mkutano huo wa kimataifa wa vijana ambayo imeahirishwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la virusi vya corona. Kwa njia hiyo Siku ya vijana ulimwenguni itafanyika jijini Lisbon 2023 nchini Ureno  na ambayo katika Nembo inaonesha rangi nyekundu na kijani pamoja na utamaduni wake wa siku ya vijana ukiwa na ishala kuu ya Bikira Maria, rangi nyeupe katika uwanja  mwekundu kukumbusha mada iliyochagaliwa na Papa Francisko kuongoza tukio hili huko Ureno isemayo “Maria aliamka na kwenda kwa haraka”

Uwasilishaji wa nembo hiyo yenye mchoro wa kuongoza Siku ya vijana, umebuniwa na msichana  mchoraji wa miaka 24 wa kireno  Beatriz Roque Antunez ambapo imewakilishwa kwa njia ya mitandao kwa kazi kubwa iliyofanyika kwani  kulikuwapo na tafsiri ya lugha 22 kupitia ukurusa wa Facebook. Kwa mujibu wa maelezo ya waandaaji wanasema ishara kuu ya nembo ni Msalaba unaoipitiwa katikati na barabara ambayo Roho Mtakatifu anabubujika ndani mwake. Na ni mwaliko kwa vijana wasisimame lakini wao wawe ndiyo wahusika wakuu wa kujenga ulimwengu wa haki na kindugu zaidi. Kwa kuongezea rangi nyekundu na kijani na rangi laini ya njano inakamilisha kwa mbali  na kuibua bendera ya Ureno.

Katika nembo hiyo, kwa mujibu wa barua rasmi inabainisha, wasifu wa Bikira Maria  na kuonesha ujana wa miaka yake, tabia ya mtu ambaye bado hajawa mama, lakini ambaye anabeba mwanga wa ulimwengu ndani yake. Na harakati ya Maria kuelekea kwa binamu yake Elizabeth, kulingana na sentensi iliyochukuliwa kutoka Injili ya Luka, ambayo inasisitizia mwaliko ulioelekezwa kwa vijana ili kuongeza nguvu zao za ndani, ndoto zao, shauku, matumaini na shukrani.  Kwa kuongeza mtunzi wa nembo hiyo ambaye anafanya kazi katika shirika la mawasiliano Ureno  amesema ni mwaliko wa kuhakikisha kuwa kitu fulani kinatokea, ni cha kujenga ulimwengu na siyo kuuacha mikononi mwa wengine. Hatimaye kuna usanii wa Rozari badala yake amesema inakusudia kusherehekea hali ya kiroho ya watu wa Mungu wa Ureno katika kujitoa kwao kwa Mama yetu wa Fatima.

Hata hivyo tarehe ya 16 ilichaguliwa si kwa bahati mbaya bali ni kama kuenzi Mtakatifu Yohane  Paulo II, mwanzilishi wa Siku za Vijana Duniani, ambapo ilikuwa tarehe 16 Oktoba 1978 alipochaguliwa kuwa Papa kuliongoza kanisa la Mungu. Nembo ya mshindi, imetangazwa,na ni matokeo ya mashindano ya kimataifa yaliyo hamasishwa  na kamati ya ndani ya maadalizi, ambapo mamia ya washindani kutoka nchi 30 za  mabara yote walishiriki. Timu kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha Ureno baadaye kilichagua mapendekezo 21 yaliyo bora zaidi, ambayo yalichunguzwa na wataalamu wa masoko na mashirika ya mawasiliano ya Ureno, na ambayo baadaye walichagua washiriki watatu tu wa mwisho. Baraza la Kipapa la Walei, familia na ndoa baadaye wamechagua pendekezo la mtu mmoja Roque Antunez kuwa mshindi bora! Taarifa ya kamati ya maandalizi mahalia imehitimisha kwa kukumbusha juu ya jitihada zilizowekwa kujiandaa pamoja na majimbo ya Ureno na kuhusu mfululizo wa mipango ya mikutano itakayofanyika kulingana na kaulimbiu ya Maria 'aliinuka akaenda kwa haraka' kwa kuzingatia maadhimisho kufanyika kijimbo kwa maandalizi ya miaka mitatu.

16 October 2020, 14:26